Sefania 2:14 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Na makundi ya wanyama watalala kati yake, wanyama wote wa mataifa; bundi na kunguru watakaa juu ya vichwa vya nguzo zake; sauti yao itasikiwa madirishani; vizingitini mwake mtakuwa ukiwa; kwa maana ameifunua kazi ya mierezi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Makundi ya mifugo yatalala humo, kadhalika kila mnyama wa porini. Tai na yangeyange na korongo wataishi juu ya nguzo zake, bundi watalia kwenye madirisha yake, kunguru watalia kwenye vizingiti, maana nyumba zake za mierezi zitakuwa tupu. Biblia Habari Njema - BHND Makundi ya mifugo yatalala humo, kadhalika kila mnyama wa porini. Tai na yangeyange na korongo wataishi juu ya nguzo zake, bundi watalia kwenye madirisha yake, kunguru watalia kwenye vizingiti, maana nyumba zake za mierezi zitakuwa tupu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Makundi ya mifugo yatalala humo, kadhalika kila mnyama wa porini. Tai na yangeyange na korongo wataishi juu ya nguzo zake, bundi watalia kwenye madirisha yake, kunguru watalia kwenye vizingiti, maana nyumba zake za mierezi zitakuwa tupu. Neno: Bibilia Takatifu Makundi ya kondoo na ng’ombe yatajilaza pale, viumbe vya kila aina. Bundi wa jangwani na bundi waliao kwa sauti nyembamba wataishi juu ya nguzo zake. Mwangwi wa kuita kwao utapita madirishani, kifusi kitakuwa milangoni, boriti za mwerezi zitaachwa wazi. Neno: Maandiko Matakatifu Makundi ya kondoo na ng’ombe yatajilaza pale, viumbe vya kila aina. Bundi wa jangwani na bundi waliao kwa sauti nyembamba wataishi juu ya nguzo zake. Mwangwi wa kuita kwao utapita madirishani, kifusi kitakuwa milangoni, boriti za mierezi zitaachwa wazi. BIBLIA KISWAHILI Na makundi ya wanyama watalala kati yake, wanyama wote wa mataifa; bundi na kunguru watakaa juu ya vichwa vya nguzo zake; sauti yao itasikiwa madirishani; vizingitini mwake mtakuwa ukiwa; kwa maana ameifunua kazi ya mierezi. |
Tena nitaifanya hiyo nchi kuwa makao ya nungunungu, na maziwa ya maji; nami nitaifagilia mbali kwa ufagio wa uharibifu; asema BWANA wa majeshi.
Asemaye, Nitajijengea nyumba kubwa yenye vyumba vipana; Naye hujikatia madirisha; Na kuta zake zimefunikwa kwa mierezi, Na kupakwa rangi nyekundu.
Nilimwona Bwana akisimama karibu na madhabahu; akasema, Vipige vichwa vya nguzo, hata vizingiti vitikisike; vivunje vipande vipande juu ya kichwa cha kila mmoja wao; nami nitamwua mtu wa mwisho wao kwa upanga; hapana hata mmoja wao atakayekimbia, wala hataokoka hata mmoja wao.
Na hiyo nchi ya pwani itakuwa malisho, yenye vibanda vya wachungaji, na mazizi ya makundi ya kondoo.
Akalia kwa sauti kuu, akisema, Umeanguka, umeanguka Babeli ulio mkuu; umekuwa maskani ya mashetani, na ngome ya kila roho mchafu, na ngome ya kila ndege mchafu mwenye kuchukiza;