Basi akamfukuza huyo mtu, akaweka Makerubi, upande wa mashariki wa bustani ya Edeni, na upanga wa moto uliogeuka huku na huko, kuilinda njia ya mti wa uzima.
Nahumu 3:3 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC mpanda farasi akipanda, na upanga ukimetameta, na mkuki ukimeremeta; na wingi wa waliouawa, na rundo kubwa la mizoga; mizoga isiyo na mwisho; wanajikwaa juu ya mizoga yao. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wapandafarasi wanashambulia, panga na mikuki inametameta; waliouawa hawana idadi, maiti wengi sana; watu wanajikwaa juu ya maiti! Biblia Habari Njema - BHND Wapandafarasi wanashambulia, panga na mikuki inametameta; waliouawa hawana idadi, maiti wengi sana; watu wanajikwaa juu ya maiti! Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wapandafarasi wanashambulia, panga na mikuki inametameta; waliouawa hawana idadi, maiti wengi sana; watu wanajikwaa juu ya maiti! Neno: Bibilia Takatifu Wapanda farasi wanaenda mbio, panga zinametameta, na mikuki inang’aa! Majeruhi wengi, malundo ya maiti, idadi ya miili isiyohesabika, watu wanajikwaa juu ya mizoga: Neno: Maandiko Matakatifu Wapanda farasi wanaenda mbio, panga zinameremeta, na mikuki inang’aa! Majeruhi wengi, malundo ya maiti, idadi kubwa ya miili isiyohesabika, watu wanajikwaa juu ya mizoga: BIBLIA KISWAHILI mpanda farasi akipanda, na upanga ukimetameta, na mkuki ukimeremeta; na wingi wa waliouawa, na rundo kubwa la mizoga; mizoga isiyo na mwisho; wanajikwaa juu ya mizoga yao. |
Basi akamfukuza huyo mtu, akaweka Makerubi, upande wa mashariki wa bustani ya Edeni, na upanga wa moto uliogeuka huku na huko, kuilinda njia ya mti wa uzima.
Ikawa usiku uo huo malaika wa BWANA alitoka, akakiingia kituo cha Waashuri, akawapiga watu mia moja themanini na tano elfu. Na watu walipoamka asubuhi na mapema, kumbe! Hao walikuwa maiti wote pia.
Watu wao waliouawa watatupwa nje, na uvundo wa maiti zao utapaa juu, na milima itayeyushwa kwa damu yao.
Basi malaika wa BWANA alitoka, akaua watu elfu mia moja na themanini na tano katika kituo cha Waashuri, na watu walipoamka asubuhi na mapema, kumbe, hao walikuwa maiti wote pia.
Kwa maana BWANA atatoa hukumu kwa watu wote kwa moto, na kwa upanga wake, nao watakaouawa na BWANA watakuwa wengi.
Utaanguka juu ya milima ya Israeli, wewe, na vikosi vyako vyote, na watu wa kabila nyingi walio pamoja nawe; nami nitakutoa na kuwapa ndege wa kila namna walao nyama, na wanyama wa pori, uliwe na wao.
Nao wataangukiana wenyewe kwa wenyewe, kama mbele ya upanga, hapo ambapo hapana afukuzaye; wala hamtakuwa na nguvu za kusimama mbele ya adui zenu.
Magari ya vita yanafanya vishindo njiani, Yanasonganasongana katika njia kuu; Kuonekana kwake ni kama mienge, Yanakwenda upesi kama umeme.
Jua na mwezi vikasimama makaoni mwao; Mbele ya nuru ya mishale yako ilipotapakaa, Mbele ya mwangaza wa mkuki wako umeremetao.