Maana silaha zote za mtu mwenye silaha wakati wa mshindo, na mavazi yaliyovingirishwa katika damu, yatakuwa tayari kuteketezwa, yatakuwa kuni za kutiwa motoni.
Nahumu 3:2 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Kelele za mjeledi, kelele za magurudumu yafanyayo kishindo; na farasi wenye kuparapara, na magari ya vita yenye kurukaruka; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Sikia! Mlio wa mjeledi, mrindimo wa magurudumu, vishindo vya farasi na ngurumo za magari! Biblia Habari Njema - BHND Sikia! Mlio wa mjeledi, mrindimo wa magurudumu, vishindo vya farasi na ngurumo za magari! Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Sikia! Mlio wa mjeledi, mrindimo wa magurudumu, vishindo vya farasi na ngurumo za magari! Neno: Bibilia Takatifu Kelele za mijeledi, vishindo vya magurudumu, farasi wanaoenda mbio na mshtuo wa magari ya vita! Neno: Maandiko Matakatifu Kelele za mijeledi, vishindo vya magurudumu, farasi waendao mbio na mshtuo wa magari ya vita! BIBLIA KISWAHILI Kelele za mjeledi, kelele za magurudumu yafanyayo kishindo; na farasi wenye kuparapara, na magari ya vita yenye kurukaruka; |
Maana silaha zote za mtu mwenye silaha wakati wa mshindo, na mavazi yaliyovingirishwa katika damu, yatakuwa tayari kuteketezwa, yatakuwa kuni za kutiwa motoni.
Kwa sababu ya kishindo cha kukanyaga kwa kwato za farasi wake walio hodari, kwa sababu ya mwendo wa mbio mbio wa magari yake ya vita; kwa sababu ya mngurumo wa magurudumu yake, hao akina baba hawatazami nyuma ili kuwaangalia watoto wao, kwa kuwa mikono yao ni dhaifu;
Kuonekana kwao ni kama kuonekana kwa farasi; na kama wapanda farasi ndivyo wanavyopiga mbio.
Kama mshindo wa magari ya vita juu ya vilele vya milima, ndivyo warukavyo; kama mshindo wa miali ya moto iunguzapo mabua makavu, kama mashujaa waliopangwa tayari kwa vita.
Kisha, kwa kishindo kwato za farasi zilipigapiga, Kwa maana walivyoenda shoti, Walipowakimbiza farasi wenye nguvu.