Itwekeni bendera katika nchi, pigeni tarumbeta kati ya mataifa, yawekeni mataifa tayari juu yake; ziiteni juu yake falme za Ararati, na Mini, na Ashkenazi; agizeni jemadari juu yake; wapandisheni farasi, kama tunutu.
Nahumu 3:17 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Watu wako waliotiwa taji ni kama nzige, na majemadari wako ni kama makundi ya mapanzi, watuao katika vitalu siku ya baridi, lakini jua lipandapo huruka juu na kwenda zao, wala hapana ajuaye walikokwenda. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wakuu wako ni kama panzi, maofisa wako kama kundi la nzige; wakati wa baridi wanakaa kwenye kuta, lakini jua lichomozapo, huruka, wala hakuna ajuaye walikokwenda. Biblia Habari Njema - BHND Wakuu wako ni kama panzi, maofisa wako kama kundi la nzige; wakati wa baridi wanakaa kwenye kuta, lakini jua lichomozapo, huruka, wala hakuna ajuaye walikokwenda. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wakuu wako ni kama panzi, maofisa wako kama kundi la nzige; wakati wa baridi wanakaa kwenye kuta, lakini jua lichomozapo, huruka, wala hakuna ajuaye walikokwenda. Neno: Bibilia Takatifu Walinzi wako ni kama nzige, maafisa wako kama makundi ya nzige wanaotua kwenye kuta wakati wa siku ya baridi; lakini wakati jua linapotokea wanaruka kwenda zao, na hakuna anayejua wanakoenda. Neno: Maandiko Matakatifu Walinzi wako ni kama nzige, maafisa wako ni kama makundi ya nzige watuao kwenye kuta wakati wa siku ya baridi: lakini wakati jua linapotokea wanaruka kwenda zao, na hakuna ajuaye waendako. BIBLIA KISWAHILI Watu wako waliotiwa taji ni kama nzige, na majemadari wako ni kama makundi ya mapanzi, watuao katika vitalu siku ya baridi, lakini jua lipandapo huruka juu na kwenda zao, wala hapana ajuaye walikokwenda. |
Itwekeni bendera katika nchi, pigeni tarumbeta kati ya mataifa, yawekeni mataifa tayari juu yake; ziiteni juu yake falme za Ararati, na Mini, na Ashkenazi; agizeni jemadari juu yake; wapandisheni farasi, kama tunutu.
Na wageni, watu wa mataifa watishao, wamemkatilia mbali na kumwacha; juu ya milima na katika mabonde yote matawi yake yameanguka, na vitanzu vyake vimevunjika karibu na mifereji yote ya nchi; na watu wote wa dunia wameshuka, wakitoka katika uvuli wake na kumwacha.
Chukueni nyara za fedha; Chukueni nyara za dhahabu; Kwa maana ni akiba isiyoisha, Fahari ya vyombo vipendezavyo.
Na maumbo ya hao nzige yalikuwa kama farasi waliowekwa tayari kwa vita, na juu ya vichwa vyao kama mataji, mfano wa dhahabu, na nyuso zao zilikuwa kama nyuso za wanadamu.