Biblia ya mtandaoni

Matangazo

Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya

Nahumu 2:3 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

Ngao ya mashujaa wake imefanywa kuwa nyekundu, watu walio hodari wa vita wamevaa nguo nyekundu sana; magari ya vita yametameta kwa chuma cha pua siku ya kukusanywa kwake, na mikuki inatikiswa kwa namna ya kutisha.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Ngao za mashujaa wake ni nyekundu, askari wake wamevaa mavazi mekundu sana. Magari yao ya farasi yanamulika kama miali ya moto, yamepangwa tayari kushambulia; farasi hawatulii kwa uchu wa kushambulia.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Ngao za mashujaa wake ni nyekundu, askari wake wamevaa mavazi mekundu sana. Magari yao ya farasi yanamulika kama miali ya moto, yamepangwa tayari kushambulia; farasi hawatulii kwa uchu wa kushambulia.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Ngao za mashujaa wake ni nyekundu, askari wake wamevaa mavazi mekundu sana. Magari yao ya farasi yanamulika kama miali ya moto, yamepangwa tayari kushambulia; farasi hawatulii kwa uchu wa kushambulia.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Ngao za askari wake ni nyekundu, mashujaa wamevaa nguo nyekundu. Chuma kwenye magari ya vita chametameta, katika siku aliyoyaweka tayari, mikuki ya msunobari inametameta.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Ngao za askari wake ni nyekundu, mashujaa wamevaa nguo nyekundu. Chuma kwenye magari ya vita chametameta, katika siku aliyoyaweka tayari, mikuki ya mierezi inametameta.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Ngao ya mashujaa wake imefanywa kuwa nyekundu, watu walio hodari wa vita wamevaa nguo nyekundu sana; magari ya vita yametameta kwa chuma cha pua siku ya kukusanywa kwake, na mikuki inatikiswa kwa namna ya kutisha.

Tazama sura
Tafsiri zingine

Nahumu 2:3
13 Marejeleo ya Msalaba  

Podo humpigia makelele, Mkuki ung'aao na fumo.

Nguruwe wa msituni wanauharibu, Na hayawani wa kondeni wanautafuna.

Naam, misonobari inakufurahia, Na mierezi ya Lebanoni, ikisema, Tokea wakati ulipolazwa chini wewe, Hapana mkata miti aliyetujia.

Nao watakuja kwako na silaha zao, na magari ya vita, na magurudumu, na wingi wa mataifa; watajipanga juu yako kwa ngao, na vigao, na chapeo za shaba, pande zote; nami nitawapa uwezo wa kuhukumu, nao watakuhukumu kulingana na hukumu zao.

Maana Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, nitamleta Nebukadneza, mfalme wa Babeli, mfalme wa wafalme, juu ya Tiro toka kaskazini, pamoja na farasi, na magari ya vita, na wapanda farasi, na jeshi, na watu wengi.

Kelele za mjeledi, kelele za magurudumu yafanyayo kishindo; na farasi wenye kuparapara, na magari ya vita yenye kurukaruka;

Niliona wakati wa usiku, na tazama, mtu amepanda farasi mwekundu, akasimama kati ya miti ya mihadasi iliyokuwa mahali penye uvuli; na nyuma yake walikuwapo farasi wengine wekundu, na wa rangi ya kijivujivu, na weupe.

Piga yowe, msonobari, maana mwerezi umeanguka, Kwa sababu miti iliyo mizuri imeharibika; Pigeni yowe, enyi mialoni ya Bashani, Kwa maana msitu wenye nguvu umeangamia.

Katika gari la kwanza walikuwa farasi wekundu; na katika gari la pili walikuwa farasi weusi;

Ikaonekana ishara nyingine mbinguni; na tazama, joka kubwa jekundu, lilikuwa na vichwa saba na pembe kumi, na juu ya vichwa vyake vilemba saba.

Akatoka farasi mwingine, mwekundu sana, na yeye aliyempanda aliruhusiwa kuiondoa amani katika nchi, ili watu wauane, naye akapewa upanga mkubwa.