Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Nahumu 1:9 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

Mnawaza nini juu ya BWANA? Yeye atakomesha kabisa; mateso hayatainuka mara ya pili.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Mbona mnafanya mipango dhidi ya Mwenyezi-Mungu? Yeye atawakomesha na kuwaangamiza, wala mpinzani wake hataweza kuinuka tena.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Mbona mnafanya mipango dhidi ya Mwenyezi-Mungu? Yeye atawakomesha na kuwaangamiza, wala mpinzani wake hataweza kuinuka tena.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Mbona mnafanya mipango dhidi ya Mwenyezi-Mungu? Yeye atawakomesha na kuwaangamiza, wala mpinzani wake hataweza kuinuka tena.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Kila njama wanayopanga dhidi ya Mwenyezi Mungu yeye atalikomesha; taabu haitatokea mara ya pili.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Shauri baya lolote wapangalo dhidi ya bwana yeye atalikomesha; taabu haitatokea mara ya pili.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Mnawaza nini juu ya BWANA? Yeye atakomesha kabisa; mateso hayatainuka mara ya pili.

Tazama sura
Tafsiri zingine



Nahumu 1:9
17 Marejeleo ya Msalaba  

Wala Amasa hakuangalia huo upanga uliomo mkononi mwa Yoabu; basi akampiga nao tumboni, akamwaga matumbo yake chini, asimpige mara ya pili; naye akafa. Kisha Yoabu na Abishai, nduguye, wakamfuata Sheba, mwana wa Bikri.


Wakipanga kukutenda mabaya, Kwa miango ya hila, hawatafanikiwa.


BWANA huyabatilisha mashauri ya mataifa, Huitangua mipango ya watu.


Hapana hekima, wala ufahamu, Wala shauri, juu ya BWANA.


Basi sasa msiwe watu wenye kudharau, vifungo vyenu msije vikakazwa; maana nimesikia kwa Bwana, BWANA wa majeshi, habari ya hukumu itakayotimizwa, nayo imekusudiwa, itakayoipata dunia yote pia.


nawe utasema, Hivyo ndivyo utakavyozama Babeli, wala hautazuka tena, kwa sababu ya mabaya yote nitakayoleta juu yake; nao watachoka. Maneno ya Yeremia yamefika hata hapa.


na watu wote wenye mwili watajua ya kuwa mimi, BWANA, nimeufuta upanga wangu alani mwake; hautarudi tena.


Bwana MUNGU asema hivi; Ni jambo baya, jambo baya la namna ya peke yake; angalia, linakuja.


Ingawa nimewafundisha na kuwatia nguvu mikono yao, hata hivyo hukusudia udhalimu juu yangu.


Ametoka mmoja kwako, akusudiaye mabaya juu ya BWANA, atoaye mashauri yasiyofaa kitu.


tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu; na tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo;


Ndipo Abishai akamwambia Daudi, Mungu amemtia adui yako mikononi mwako leo; basi, niache nimpige kwa hilo fumo hadi chini kwa pigo moja, sitampiga mara ya pili.


Siku hiyo nitayatimiza maneno yale yote niliyoyasema juu ya Eli kuhusu nyumba yake, tangu mwanzo hadi mwisho.