Nahumu 1:15 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Tazama, juu ya milima iko miguu yake aletaye habari njema, atangazaye amani. Zishike sikukuu zako, Ee Yuda, uziondoe nadhiri zako; kwa maana yule asiyefaa kitu hatapita kati yako tena kamwe; amekwisha kukatiliwa mbali. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Enyi watu wa Yuda tazameni: Anakuja kutoka mlimani mtu anayeleta habari njema, mjumbe ambaye anatangaza amani. Adhimisheni sikukuu zenu, enyi watu wa Yuda, timizeni nadhiri zenu, maana waovu hawatawavamia tena, kwani wameangamizwa kabisa. Biblia Habari Njema - BHND Enyi watu wa Yuda tazameni: Anakuja kutoka mlimani mtu anayeleta habari njema, mjumbe ambaye anatangaza amani. Adhimisheni sikukuu zenu, enyi watu wa Yuda, timizeni nadhiri zenu, maana waovu hawatawavamia tena, kwani wameangamizwa kabisa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Enyi watu wa Yuda tazameni: Anakuja kutoka mlimani mtu anayeleta habari njema, mjumbe ambaye anatangaza amani. Adhimisheni sikukuu zenu, enyi watu wa Yuda, timizeni nadhiri zenu, maana waovu hawatawavamia tena, kwani wameangamizwa kabisa. Neno: Bibilia Takatifu Tazama, huko juu milimani, miguu ya huyo mmoja aletaye habari njema, ambaye anatangaza amani! Ee Yuda, sherehekea sikukuu zako, nawe utimize nadhiri zako. Waovu hawatakuvamia tena; wataangamizwa kabisa. Neno: Maandiko Matakatifu Tazama, huko juu milimani, miguu ya huyo mmoja aletaye habari njema, ambaye anatangaza amani! Ee Yuda, sherehekea sikukuu zako, nawe utimize nadhiri zako. Waovu hawatakuvamia tena; wataangamizwa kabisa. BIBLIA KISWAHILI Tazama, juu ya milima iko miguu yake aletaye habari njema, atangazaye amani. Zishike sikukuu zako, Ee Yuda, uziondoe nadhiri zako; kwa maana yule asiyefaa kitu hatapita kati yako tena kamwe; amekwisha kukatiliwa mbali. |
Mimi kwanza nitauambia Sayuni, Tazama; hawa ndio; nami nitampa Yerusalemu mletaji wa habari njema.
Jangwa na miji yake na ipaze sauti zao, Vijiji vinavyokaliwa na Kedari; Na waimbe wenyeji wa Sela, Wapige kelele toka vilele vya milima.
Amka, amka, jivike nguvu zako, Ee Sayuni; Jivike mavazi yako mazuri, Ee Yerusalemu, mji mtakatifu; Kwa maana tokea sasa hataingia ndani yako Asiyetahiriwa, wala aliye najisi.
Jinsi ilivyo mizuri juu ya milima Miguu yake aletaye habari njema, Yeye aitangazaye amani, Aletaye habari njema ya mambo mema, Yeye autangazaye wokovu, Auambiaye Sayuni, Mungu wako anamiliki!
Hivyo ndivyo mtakavyojua ya kuwa mimi ndimi BWANA, Mungu wenu, nikaaye Sayuni, mlima wangu mtakatifu; ndipo Yerusalemu utakapokuwa mtakatifu, wala wageni hawatapita tena ndani yake kamwe.
Nena na wana wa Israeli, na kuwaambia, Sikukuu za BWANA, ambazo mtazitangaza kuwa ni makusanyiko matakatifu; hizi ni sikukuu zangu.
Sikukuu za BWANA ni hizi, ni makusanyiko matakatifu, ambayo mtayatangaza kwa nyakati zake.
Tena BWANA ametoa amri katika habari zako, ya kwamba asiwepo tena mtu awaye yote mwenye jina lako; toka nyumba ya miungu yako nitakatilia mbali sanamu ya kuchora, na sanamu ya kuyeyusha; nitakufanyia kaburi lako; kwa maana u mbovu.
Malaika akawaambia, Msiogope; kwa kuwa mimi ninawaletea habari njema ya furaha kuu itakayokuwa kwa watu wote;
Neno lile alilowapelekea wana wa Israeli akihubiri Habari Njema ya amani kwa Yesu Kristo (ndiye Bwana wa wote),
Tena wahubirije, wasipopelekwa? Kama ilivyoandikwa, Ni mizuri kama nini miguu yao wahubirio habari ya mema!