Ikawa, alipokuwa akiabudu nyumbani mwa Nisroki, mungu wake, Adrameleki na Shareza wakampiga kwa upanga; wakaikimbilia nchi ya Ararati. Na Esar-hadoni mwanawe akatawala mahali pake.
Nahumu 1:14 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Tena BWANA ametoa amri katika habari zako, ya kwamba asiwepo tena mtu awaye yote mwenye jina lako; toka nyumba ya miungu yako nitakatilia mbali sanamu ya kuchora, na sanamu ya kuyeyusha; nitakufanyia kaburi lako; kwa maana u mbovu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mwenyezi-Mungu ameamuru hivi kuhusu Ninewi: “Hutapata wazawa kulidumisha jina lako. Sanamu zako za kuchonga na za kusubu, nitazivunjavunja nyumbani mwa miungu yako. Mimi nitakuchimbia kaburi lako, maana wewe hufai kitu chochote.” Biblia Habari Njema - BHND Mwenyezi-Mungu ameamuru hivi kuhusu Ninewi: “Hutapata wazawa kulidumisha jina lako. Sanamu zako za kuchonga na za kusubu, nitazivunjavunja nyumbani mwa miungu yako. Mimi nitakuchimbia kaburi lako, maana wewe hufai kitu chochote.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mwenyezi-Mungu ameamuru hivi kuhusu Ninewi: “Hutapata wazawa kulidumisha jina lako. Sanamu zako za kuchonga na za kusubu, nitazivunjavunja nyumbani mwa miungu yako. Mimi nitakuchimbia kaburi lako, maana wewe hufai kitu chochote.” Neno: Bibilia Takatifu Hii ndiyo amri Mwenyezi Mungu aliyoitoa kukuhusu wewe, Ninawi: “Hutakuwa na wazao watakaoendeleza jina lako. Nitaharibu sanamu za kuchonga na sanamu za kusubu zilizopo katika hekalu la miungu yenu. Nitaandaa kaburi lako, kwa maana wewe ni mwovu kabisa.” Neno: Maandiko Matakatifu Hii ndiyo amri bwana aliyoitoa kukuhusu wewe, Ninawi: “Hutakuwa na wazao watakaoendeleza jina lako. Nitaharibu sanamu za kuchonga na sanamu za kuyeyusha ambazo zipo katika hekalu la miungu yenu. Nitaandaa kaburi lako, kwa maana wewe ni mwovu kabisa.” BIBLIA KISWAHILI Tena BWANA ametoa amri katika habari zako, ya kwamba asiwepo tena mtu awaye yote mwenye jina lako; toka nyumba ya miungu yako nitakatilia mbali sanamu ya kuchora, na sanamu ya kuyeyusha; nitakufanyia kaburi lako; kwa maana u mbovu. |
Ikawa, alipokuwa akiabudu nyumbani mwa Nisroki, mungu wake, Adrameleki na Shareza wakampiga kwa upanga; wakaikimbilia nchi ya Ararati. Na Esar-hadoni mwanawe akatawala mahali pake.
Naye BWANA akatuma malaika aliyewakatia mbali wapiganaji vita wote, na majemadari, na makamanda, kambini mwa mfalme wa Ashuru. Basi akarudia nchi yake kwa aibu. Naye alipoingia nyumbani mwa mungu wake, baadhi ya wanawe mwenyewe wakamwangamiza humo kwa upanga.
Uwe kwangu mwamba wa makazi yangu, Ngome imara ya wokovu wangu. Maana wewe, Ndiwe mwamba wangu na ngome yangu.
Maana nitapita kati ya nchi ya Misri usiku huo, nami nitawaua wazaliwa wa kwanza wote katika nchi ya Misri, wa mwanadamu na wa mnyama; nami nitafanya hukumu juu ya miungu yote ya Misri; Mimi ndimi BWANA.
Ufunuo juu ya Misri. Tazama, BWANA amepanda juu ya wingu jepesi, anafika Misri; na sanamu za Misri zinatikisika mbele zake, na moyo wa Misri unayeyuka ndani yake.
Tangazeni katika mataifa, Mkahubiri na kutweka bendera; Hubirini, msifiche, semeni, Babeli umetwaliwa! Beli amefedheheka; Merodaki amefadhaika; Sanamu zake zimeaibishwa, Vinyago vyake vimefadhaika.
Kisha badala yake atasimama mmoja, mtu astahiliye kudharauliwa, ambaye hawakumpa heshima ya ufalme; naye atakuja wakati wa amani, naye ataupata ufalme kwa kujipendekeza.
Nami nitapaharibu mahali penu palipoinuka, na kuziangusha sanamu zenu za jua, nami nitaitupa mizoga yenu juu ya mizoga ya sanamu zenu; na roho yangu itawachukia.
nami nitakatilia mbali sanamu zako na nguzo zako, zitoke kati yako; wala hutaiabudu tena kazi ya mikono yako.
Wewe umeifanyia nyumba yako kusudi la aibu, kwa kukatilia mbali watu wengi, nawe umetenda dhambi juu ya roho yako.
Kwa maana nimemwambia ya kwamba nitaihukumu nyumba yake milele, kwa ajili ya ule uovu alioujua; kwa kuwa wanawe walijiletea laana, wala yeye hakuwazuia.