Mungu akasema, Hii ndiyo ishara ya agano nifanyalo kati yangu na ninyi, na kila kiumbe hai kilichoko pamoja nanyi, kwa vizazi vyote hata milele;
Mwanzo 9:13 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Mimi nauweka upinde wangu winguni, nao utakuwa ni ishara ya agano kati yangu na nchi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Naweka upinde wangu mawinguni, nao utakuwa ishara ya agano kati yangu na dunia. Biblia Habari Njema - BHND Naweka upinde wangu mawinguni, nao utakuwa ishara ya agano kati yangu na dunia. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza naweka upinde wangu mawinguni, nao utakuwa ishara ya agano kati yangu na dunia. Neno: Bibilia Takatifu Nimeweka upinde wangu wa mvua mawinguni, nao utakuwa ishara ya agano nifanyalo kati yangu na dunia. Neno: Maandiko Matakatifu Nimeweka upinde wangu wa mvua mawinguni, nao utakuwa ishara ya Agano nifanyalo kati yangu na dunia. BIBLIA KISWAHILI Mimi nauweka upinde wangu winguni, nao utakuwa ni ishara ya agano kati yangu na nchi. |
Mungu akasema, Hii ndiyo ishara ya agano nifanyalo kati yangu na ninyi, na kila kiumbe hai kilichoko pamoja nanyi, kwa vizazi vyote hata milele;
Kama kuonekana kwa upinde wa mvua, ulio katika mawingu siku ya mvua, ndivyo kulivyokuwa kuonekana kwa mwangaza ule pande zote. Ndivyo kulivyokuwa kuonekana kwake mfano huo wa utukufu wa BWANA. Nami nilipoona nilianguka kifudifudi, nikasikia sauti ya mmoja anenaye.
Kisha nikaona malaika mwingine mwenye nguvu akishuka kutoka mbinguni, amevikwa wingu; na upinde wa mvua juu ya kichwa chake; na uso wake ulikuwa kama jua, na miguu yake kama nguzo za moto.
na yeye aliyeketi alionekana mithili ya jiwe la yaspi na akiki, na upinde wa mvua ulikizunguka kile kiti cha enzi, ukionekana mithili ya zumaridi.