Uifanyie safina mwangaza, ukaumalize juu kiasi cha mkono mmoja; ukautie mlango wa safina katika ubavu wake; ukaifanyie dari tatu, ya chini, ya pili, na ya tatu.
Mwanzo 8:6 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Ikawa baada ya siku arubaini, Nuhu akalifungua dirisha la safina, alilolifanya; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Baada ya siku arubaini, Noa alifungua dirisha alilokuwa ametengeneza katika hiyo safina, Biblia Habari Njema - BHND Baada ya siku arubaini, Noa alifungua dirisha alilokuwa ametengeneza katika hiyo safina, Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Baada ya siku arubaini, Noa alifungua dirisha alilokuwa ametengeneza katika hiyo safina, Neno: Bibilia Takatifu Baada ya siku arobaini, Nuhu akafungua dirisha alilokuwa amelifanya katika safina, Neno: Maandiko Matakatifu Baada ya siku arobaini Nuhu akafungua dirisha alilokuwa amelifanya katika safina BIBLIA KISWAHILI Ikawa baada ya siku arobaini, Nuhu akalifungua dirisha la safina, alilolifanya; |
Uifanyie safina mwangaza, ukaumalize juu kiasi cha mkono mmoja; ukautie mlango wa safina katika ubavu wake; ukaifanyie dari tatu, ya chini, ya pili, na ya tatu.
Maji yakapungukapunguka hata mwezi wa kumi; mwezi huo wa kumi, siku ya kwanza ya mwezi, vilele vya milima vikaonekana.
Hata Danieli, alipojua ya kuwa yale maandiko yamekwisha kutiwa sahihi, akaingia nyumbani mwake, (na madirisha katika chumba chake yalikuwa yamefunguliwa kuelekea Yerusalemu;) akapiga magoti mara tatu kila siku, akasali, akashukuru mbele za Mungu wake, kama alivyokuwa akifanya tokea hapo.