Mwanzo 50:15 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Ndugu zake Yusufu walipoona ya kwamba baba yao amekufa, walisema, Labda Yusufu atatuchukia; naye atatulipa maovu yetu tuliyomtenda. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Baada ya kifo cha baba yao, ndugu zake Yosefu walisemezana, “Huenda Yosefu atatuchukia na kutulipiza mabaya yote tuliyomtendea.” Biblia Habari Njema - BHND Baada ya kifo cha baba yao, ndugu zake Yosefu walisemezana, “Huenda Yosefu atatuchukia na kutulipiza mabaya yote tuliyomtendea.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Baada ya kifo cha baba yao, ndugu zake Yosefu walisemezana, “Huenda Yosefu atatuchukia na kutulipiza mabaya yote tuliyomtendea.” Neno: Bibilia Takatifu Ndugu zake Yusufu walipoona kwamba baba yao amekufa, wakasema, “Itakuwaje kama Yusufu ataweka kinyongo dhidi yetu na kutulipa mabaya yote tuliyomtendea?” Neno: Maandiko Matakatifu Ndugu zake Yusufu walipoona kwamba baba yao amekufa, wakasema, “Itakuwaje kama Yusufu ataweka kinyongo dhidi yetu na kutulipa mabaya yote tuliyomtendea?” BIBLIA KISWAHILI Ndugu zake Yusufu walipoona ya kwamba baba yao amekufa, walisema, Labda Yusufu atatuchukia; naye atatulipa maovu yetu tuliyomtenda. |
Wakapita wafanya biashara Wamidiani; basi wakamtoa Yusufu, wakampandisha kumtoa katika shimo, wakamuuza Yusufu kwa Waishmaeli kwa vipande vya fedha ishirini; nao wakamchukua Yusufu mpaka Misri.
Yusufu akarudi Misri, yeye na ndugu zake, na wote waliokwenda pamoja naye kumzika baba yake, baada ya kumzika baba yake.
Hapo ndipo waovu watakaposhikwa na hofu nyingi, Maana Mungu yupo pamoja na kizazi cha haki.
Hapo waliingiwa na hofu pasipokuwapo hofu, Maana Mungu ameitawanya mifupa yake aliyekuhusuru. Umewatia aibu, Kwa sababu MUNGU amewadharau.
Tena hao wa kwenu watakaobaki, nitawatia woga mioyoni mwao, katika hizo nchi za adui zao; na sauti ya jani lililopeperushwa itawakimbiza; nao watakimbia, kama mtu akimbiavyo upanga; nao wataanguka hapo ambapo hapana afukuzaye.
Hao waionesha kazi ya torati iliyoandikwa mioyoni mwao, dhamiri yao ikiwashuhudia, na mawazo yao, yenyewe kwa yenyewe, yakiwashitaki au kuwatetea;