Mwanzo 49:31 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Humo walimzika Abrahamu, na Sara mkewe; humo wakamzika Isaka, na Rebeka mkewe; nami humo nikamzika Lea; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Huko ndiko walikozikwa Abrahamu na mkewe Sara; huko ndiko walikozikwa Isaka na mkewe Rebeka; na huko ndiko nilikomzika Lea. Biblia Habari Njema - BHND Huko ndiko walikozikwa Abrahamu na mkewe Sara; huko ndiko walikozikwa Isaka na mkewe Rebeka; na huko ndiko nilikomzika Lea. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Huko ndiko walikozikwa Abrahamu na mkewe Sara; huko ndiko walikozikwa Isaka na mkewe Rebeka; na huko ndiko nilikomzika Lea. Neno: Bibilia Takatifu Huko ndiko Ibrahimu na Sara mkewe walikozikwa, huko akazikwa Isaka na Rebeka mkewe, na huko nilimzika Lea. Neno: Maandiko Matakatifu Huko ndiko Ibrahimu na Sara mkewe walikozikwa, huko akazikwa Isaka na Rebeka mkewe, na huko nilimzika Lea. BIBLIA KISWAHILI Humo walimzika Abrahamu, na Sara mkewe; humo wakamzika Isaka, na Rebeka mkewe; nami humo nikamzika Lea; |
Katika lile shamba alilolinunua Abrahamu kwa wazawa wa Hethi, huko ndiko alikozikwa Abrahamu na Sara mkewe.
Isaka na Ishmaeli wanawe wakamzika katika pango ya Makpela, katika shamba la Efroni mwana wa Sohari Mhiti, lielekealo Mamre.
Naye Isaka akakata roho, akafa, akakusanyika kwa watu wake, ni mzee, ameshiba siku. Esau na Yakobo, wanawe, wakamzika.
Lakini nitakapolala pamoja na baba zangu, unichukue toka Misri, unizike katika kaburi lao. Akasema, Nitafanya kama ulivyosema.
kwa kuwa wanawe wakamchukua mpaka nchi ya Kanaani, na wakamzika katika pango ya shamba la Makpela, iliyo mbele ya Mamre, aliyoinunua Abrahamu pamoja na shamba kwa Efroni Mhiti, pawe milki yake ya kuzikia.
wakachukuliwa mpaka Shekemu wakazikwa katika kaburi lile, ambalo Abrahamu alilinunua kwa kima fulani cha fedha kutoka kwa wana wa Hamori, huko Shekemu.