Na lile shamba, na pango lililomo, iliyakinishwa kuwa mali yake Abrahamu na wazawa wa Hethi, kuwa mahali pa kuzikia.
Mwanzo 49:30 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC katika ile pango iliyomo shambani mwa Makpela, iliyo mbele ya Mamre katika nchi ya Kanaani, aliyoinunua Abrahamu pamoja na shamba kwa Efroni Mhiti, pawe milki yake ya kuzikia. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema kule Makpela, mashariki ya Mamre, nchini Kanaani. Abrahamu alinunua pango na shamba hilo kwa Efroni, Mhiti, liwe lake la kuzikia. Biblia Habari Njema - BHND kule Makpela, mashariki ya Mamre, nchini Kanaani. Abrahamu alinunua pango na shamba hilo kwa Efroni, Mhiti, liwe lake la kuzikia. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza kule Makpela, mashariki ya Mamre, nchini Kanaani. Abrahamu alinunua pango na shamba hilo kwa Efroni, Mhiti, liwe lake la kuzikia. Neno: Bibilia Takatifu pango lililoko katika shamba la Makpela, karibu na Mamre huko Kanaani, ambalo Ibrahimu alinunua liwe mahali pa kuzikia kutoka kwa Efroni, Mhiti, pamoja na shamba. Neno: Maandiko Matakatifu pango lililoko katika shamba la Makpela, karibu na Mamre huko Kanaani, ambalo Ibrahimu alinunua kwa ajili ya mahali pa kuzikia kutoka kwa Efroni, Mhiti, pamoja na shamba. BIBLIA KISWAHILI katika lile pango lililomo shambani mwa Makpela, lililo mbele ya Mamre katika nchi ya Kanaani, alilolinunua Abrahamu pamoja na shamba kwa Efroni Mhiti, pawe milki yake ya kuzikia. |
Na lile shamba, na pango lililomo, iliyakinishwa kuwa mali yake Abrahamu na wazawa wa Hethi, kuwa mahali pa kuzikia.
Mimi ni mgeni, ninatembea kwenu; nipeni mahali pa kuzikia kwenu, pawe pangu, nimzike maiti wangu atoke mbele yangu.
Isaka na Ishmaeli wanawe wakamzika katika pango ya Makpela, katika shamba la Efroni mwana wa Sohari Mhiti, lielekealo Mamre.