Mwanzo 49:23 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Wapiga mishale walimtenda machungu, Wakamlenga na kumbana sana Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Wapiga mishale walimshambulia vikali, wakamtupia mishale na kumsumbua sana. Biblia Habari Njema - BHND “Wapiga mishale walimshambulia vikali, wakamtupia mishale na kumsumbua sana. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wapiga mishale walimshambulia vikali, wakamtupia mishale na kumsumbua sana. Neno: Bibilia Takatifu Kwa uchungu wapiga mshale walimshambulia, wakampiga mshale kwa ukatili. Neno: Maandiko Matakatifu Kwa uchungu wapiga mshale walimshambulia, wakampiga mshale kwa ukatili. BIBLIA KISWAHILI Wapiga mishale walimtenda machungu, Wakamlenga na kumbana sana |
Wakapita wafanya biashara Wamidiani; basi wakamtoa Yusufu, wakampandisha kumtoa katika shimo, wakamuuza Yusufu kwa Waishmaeli kwa vipande vya fedha ishirini; nao wakamchukua Yusufu mpaka Misri.
Ndugu zake wakaona ya kuwa baba yao anampenda kuliko ndugu zake wote, wakamchukia, wala hawakuweza kusema naye kwa amani.
Wakaambiana, Kweli sisi tulimkosea ndugu yetu, kwa kuwa tuliona shida ya roho yake, alipotusihi, wala hatukusikia, kwa hiyo shida hii imetupata.
Yusufu ni mti mchanga wenye kuzaa, Mti mchanga wenye kuzaa karibu na chemchemi, Matawi yake yametanda ukutani.
Lakini upinde wake ukakaa imara, Mikono yake ikapata nguvu, Kwa mikono ya Mwenye Enzi wa Yakobo; Kwa jina la mchungaji, yeye mwamba wa Israeli,
Hayo nimewaambieni mpate kuwa na amani ndani yangu. Ulimwenguni mnayo dhiki; lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu.
wakifanya imara roho za wanafunzi na kuwahimiza wakae katika ile Imani, na ya kwamba imetupasa kuingia katika ufalme wa Mungu kwa njia ya dhiki nyingi.