Raheli akasema, Kwa mashindano makuu nimeshindana na dada yangu, nikashinda. Akamwita jina lake Naftali.
Mwanzo 49:21 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Naftali ni ayala aliyefunguliwa; Anatoa maneno mazuri. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Naftali ni kama paa aliye huru, azaaye watoto walio wazuri. Biblia Habari Njema - BHND “Naftali ni kama paa aliye huru, azaaye watoto walio wazuri. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Naftali ni kama paa aliye huru, azaaye watoto walio wazuri. Neno: Bibilia Takatifu “Naftali ni kulungu jike aliyeachiwa huru azaaye watoto wazuri. Neno: Maandiko Matakatifu “Naftali ni kulungu jike aliyeachiwa huru azaaye watoto wazuri. BIBLIA KISWAHILI Naftali ni ayala aliyefunguliwa; Anatoa maneno mazuri. |
Raheli akasema, Kwa mashindano makuu nimeshindana na dada yangu, nikashinda. Akamwita jina lake Naftali.
Wakamwambia, wakasema, Ukiwa mwema kwao watu hawa, na kuwapendeza, na kuwaambia maneno mazuri, hapo watakuwa watumishi wako siku zote.
Ni ayala apendaye na paa apendezaye; Matiti yake yakutoshe sikuzote; Na kwa upendo wake ushangilie daima.
Nawasihi, enyi binti za Yerusalemu, Kwa paa na kwa ayala wa porini, Msiyachochee mapenzi, wala kuyaamsha, Hata yatakapoona vema yenyewe.
Na Naftali akamnena, Ee Naftali, uliyeshiba fadhili, Uliyejawa na baraka ya BWANA; Umiliki magharibi na kusini.
Baraka akawakutanisha Naftali na Zabuloni waende Kedeshi wakakwea watu elfu kumi wakimfuata; Debora naye akaenda pamoja naye.
Siku moja Debora akatuma mtu akamwita Baraka wa Abinoamu kutoka Kedesh-Naftali, akamwambia, BWANA, Mungu wa Israeli anakuamuru hivi: “Nenda, ukawaogoze watu elfu kumi na wana wa Naftali, na wa wana wa Zabuloni, ili washike doria katika mlima Tabori”.
Zabuloni ndio watu waliohatarisha roho zao hadi kufa; Nao Naftali mahali palipoinuka kondeni.