Mwanzo 49:19 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Gadi, jeshi litamsonga, Lakini atawasonga wao mpaka visigino. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Gadi atashambuliwa na wanyanganyi, lakini yeye atawafuata nyuma na kuwashambulia. Biblia Habari Njema - BHND “Gadi atashambuliwa na wanyanganyi, lakini yeye atawafuata nyuma na kuwashambulia. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Gadi atashambuliwa na wanyang'anyi, lakini yeye atawafuata nyuma na kuwashambulia. Neno: Bibilia Takatifu “Gadi atashambuliwa ghafula na kundi la washambuliaji, lakini yeye atawageukia na kuwashinda kabisa. Neno: Maandiko Matakatifu “Gadi atashambuliwa ghafula na kundi la washambuliaji, lakini yeye atawageukia na kuwashinda kabisa. BIBLIA KISWAHILI Gadi, jeshi litamsonga, Lakini atawasonga wao mpaka visigino. |
Naye Mungu wa Israeli akamwamsha roho Pulu, mfalme wa Ashuru, yaani roho ya Tiglath-Pileseri, mfalme wa Ashuru, naye akawachukua mateka hao Wareubeni, na Wagadi, na nusu kabila ya Wamanase; akawaleta mpaka Hala, na Habori, na Hara, na mpaka mto wa Gozani, hata siku hii ya leo.
Pamoja na yeye, Wareubeni na Wagadi walipata urithi wao, waliopewa na Musa, huko ng'ambo ya Yordani upande wa mashariki, vile vile kama huyo Musa mtumishi wa BWANA alivyowapa;