Wakambariki Rebeka, wakamwambia, Dada yetu, wewe uwe mama wa elfu kumi, mara elfu nyingi, na wazao wako waurithi mlango wa hao wawachukiao.
Mwanzo 48:20 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Akawabariki siku ile akisema, Katika ninyi Waisraeli watabariki, wakisema, Mungu na akufanye kama Efraimu na kama Manase. Akamweka Efraimu mbele ya Manase. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Basi, Israeli akawabariki siku hiyo, akisema, “Waisraeli watayatumia majina yenu kubarikia, watasema, ‘Mungu akutendee mema kama Efraimu na Manase!’” Ndivyo Israeli alivyomweka Efraimu mbele ya Manase. Biblia Habari Njema - BHND Basi, Israeli akawabariki siku hiyo, akisema, “Waisraeli watayatumia majina yenu kubarikia, watasema, ‘Mungu akutendee mema kama Efraimu na Manase!’” Ndivyo Israeli alivyomweka Efraimu mbele ya Manase. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Basi, Israeli akawabariki siku hiyo, akisema, “Waisraeli watayatumia majina yenu kubarikia, watasema, ‘Mungu akutendee mema kama Efraimu na Manase!’” Ndivyo Israeli alivyomweka Efraimu mbele ya Manase. Neno: Bibilia Takatifu Akawabariki siku ile na kusema, “Kwa jina lenu Israeli watatamka baraka hii: ‘Mungu na awafanye kama Efraimu na Manase.’ ” Kwa hiyo akamtanguliza Efraimu mbele ya Manase. Neno: Maandiko Matakatifu Akawabarikia siku ile na kusema, “Kwa jina lenu Israeli watatamka baraka hii: ‘Mungu na awafanye kama Efraimu na Manase.’ ” Kwa hiyo akamtanguliza Efraimu mbele ya Manase. BIBLIA KISWAHILI Akawabariki siku ile akisema, Katika ninyi Waisraeli watabariki, wakisema, Mungu na akufanye kama Efraimu na kama Manase. Akamweka Efraimu mbele ya Manase. |
Wakambariki Rebeka, wakamwambia, Dada yetu, wewe uwe mama wa elfu kumi, mara elfu nyingi, na wazao wako waurithi mlango wa hao wawachukiao.
Israeli akamwambia Yusufu, Angalia, mimi ninakufa, lakini Mungu atakuwa pamoja nanyi, naye atawarudisha mpaka nchi ya baba zenu.
Hayo ndiyo majina ya hao watu waliotumwa na Musa waende kuipeleleza nchi. Na huyo Hoshea mwana wa Nuni, Musa akamwita jina lake Yoshua.
Kwa imani Yakobo, alipokuwa karibu kufa, akambariki kila mmoja wa wana wa Yusufu, akaabudu akiegemea kichwa cha fimbo yake.
Kisha wana wa Yusufu wakanena na Yoshua, wakasema, Kwa nini umenipa mimi sehemu moja tu na fungu moja kuwa ni urithi wangu, kwa kuwa mimi ni taifa kubwa la watu, kwa sababu BWANA amenibariki hata hivi sasa?