Shemu akaishi baada ya kumzaa Arfaksadi miaka mia tano, akazaa wana, wa kiume na wa kike.
Mwanzo 47:9 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Yakobo akamjibu Farao, Siku za kuishi kwangu ni miaka mia moja na thelathini; siku za maisha yangu zimekuwa chache, tena za taabu, wala hazikufikia siku za maisha ya baba zangu katika siku za kuishi kwao. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Yakobo akamjibu, “Umri niliojaliwa kama msafiri ni miaka 130. Miaka hiyo imekuwa michache na iliyojaa mateso, tena haijafikia idadi ya miaka waliyoishi wazee wangu kama wasafiri.” Biblia Habari Njema - BHND Yakobo akamjibu, “Umri niliojaliwa kama msafiri ni miaka 130. Miaka hiyo imekuwa michache na iliyojaa mateso, tena haijafikia idadi ya miaka waliyoishi wazee wangu kama wasafiri.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Yakobo akamjibu, “Umri niliojaliwa kama msafiri ni miaka 130. Miaka hiyo imekuwa michache na iliyojaa mateso, tena haijafikia idadi ya miaka waliyoishi wazee wangu kama wasafiri.” Neno: Bibilia Takatifu Naye Yakobo akamwambia Farao, “Siku za miaka ya kusafiri kwangu ni miaka mia moja na thelathini. Miaka yangu imekuwa michache na ya taabu, wala haikufikia miaka ya maisha ya baba zangu.” Neno: Maandiko Matakatifu Naye Yakobo akamwambia Farao, “Siku za miaka ya kusafiri kwangu ni miaka 130. Miaka yangu imekuwa michache na ya taabu, wala haikufikia miaka ya kusafiri ya baba zangu.” BIBLIA KISWAHILI Yakobo akamjibu Farao, Siku za kuishi kwangu ni miaka mia moja na thelathini; siku za maisha yangu zimekuwa chache, tena za taabu, wala hazikufikia siku za maisha ya baba zangu katika siku za kuishi kwao. |
Shemu akaishi baada ya kumzaa Arfaksadi miaka mia tano, akazaa wana, wa kiume na wa kike.
Yakobo akaishi katika nchi ya Misri miaka kumi na saba, basi umri wake Yakobo ulikuwa miaka mia moja na arubaini na saba.
Basi Yusufu akafa, mwenye miaka mia moja na kumi; wakampaka dawa, wakamtia katika sanduku, huko Misri.
Kwani sisi tu wageni na wapitaji mbele zako, kama walivyokuwa baba zetu wote; siku zetu duniani ni kama kivuli, na hakuna tumaini la kuishi.
Ee BWANA, usikie maombi yangu, Utege sikio lako niliapo, Usiyapuuze machozi yangu. Kwa maana mimi ni mgeni wako, Msafiri kama baba zangu wote.
Tazama, umefanya siku zangu kuwa mashubiri; Maisha yangu ni kama si kitu mbele zako. Kila mwanadamu, ingawa amesitawi, ni ubatili.
Tena nimelithibitisha agano langu nao, la kuwapa nchi ya Kanaani; nchi ya waliyokaa kama wageni.
Huyo Musa alikuwa ni mtu wa miaka themanini umri wake, na Haruni alikuwa ni mtu wa miaka themanini na mitatu, hapo waliponena na Farao.
Basi siku zote tuna moyo mkuu; tena twajua ya kuwa, wakati tuwapo hapa katika mwili, tunakaa mbali na Bwana.
Musa alikuwa mtu wa miaka mia moja na ishirini alipokufa; jicho lake halikupofuka, wala nguvu za mwili wake hazikupunguka.
lakini hamjui yatakayokuwako kesho. Uzima wenu ni nini? Maana ninyi ni mvuke uonekanao kwa muda mfupi tu, kisha hutoweka.
Ikawa, baada ya hayo, Yoshua, mwana wa Nuni, mtumishi wa BWANA, akafa, mwenye umri wa miaka mia moja na kumi.
Wapenzi, nawasihi kama wapitaji na wasafiri, ziepukeni tamaa za mwili zipiganazo na roho.