Farao akamwita Yusufu, Safenath-panea; akamwoza Asenathi, binti Potifera, kuhani wa Oni, kuwa mkewe. Na Yusufu akaenda huku na huko katika nchi yote ya Misri.
Mwanzo 46:20 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Walizaliwa kwake Yusufu katika nchi ya Misri, Manase na Efraimu, aliomzalia Asenathi binti Potifera, kuhani wa Oni. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Huko Misri, Asenathi, binti Potifera, aliyekuwa kuhani wa mji wa Oni, alimzalia Yosefu wana wawili: Manase na Efraimu. Biblia Habari Njema - BHND Huko Misri, Asenathi, binti Potifera, aliyekuwa kuhani wa mji wa Oni, alimzalia Yosefu wana wawili: Manase na Efraimu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Huko Misri, Asenathi, binti Potifera, aliyekuwa kuhani wa mji wa Oni, alimzalia Yosefu wana wawili: Manase na Efraimu. Neno: Bibilia Takatifu Huko Misri, Asenathi binti Potifera, aliyekuwa kuhani wa mji wa Oni, alimzalia Yusufu wana wawili: Manase na Efraimu. Neno: Maandiko Matakatifu Huko Misri, Asenathi binti wa Potifera, aliyekuwa kuhani wa mji wa Oni, alimzalia Yusufu wana wawili, Manase na Efraimu. BIBLIA KISWAHILI Walizaliwa kwake Yusufu katika nchi ya Misri, Manase na Efraimu, aliomzalia Asenathi binti Potifera, kuhani wa Oni. |
Farao akamwita Yusufu, Safenath-panea; akamwoza Asenathi, binti Potifera, kuhani wa Oni, kuwa mkewe. Na Yusufu akaenda huku na huko katika nchi yote ya Misri.
Ikawa, baada ya mambo hayo, Yusufu akaambiwa, Tazama, baba yako ni mgonjwa; akawatwaa wanawe wawili, Manase na Efraimu, pamoja naye.
Akawabariki siku ile akisema, Katika ninyi Waisraeli watabariki, wakisema, Mungu na akufanye kama Efraimu na kama Manase. Akamweka Efraimu mbele ya Manase.
Vijana wa Oni, na wa Pi-besethi, wataanguka kwa upanga; na miji hiyo itakwenda utumwani.
Kwa kuwa wana wa Yusufu walikuwa makabila mawili, Manase na Efraimu; nao hawakuwapa Walawi sehemu katika hiyo nchi, isipokuwa waliwapa miji wapate kuikaa, pamoja na viunga vyake kwa ajili ya mifugo wao, na kwa ajili ya riziki zao.
Hii ndiyo sehemu waliyopewa kabila la Manase; maana, yeye alikuwa ni mzaliwa wa kwanza, wa Yusufu. Na Makiri, mzaliwa wa kwanza wa Manase, babaye Gileadi, kwa sababu alikuwa mtu wa vita, basi alikuwa na Gileadi na Bashani.