Mtabainika kwa njia hii; aishivyo Farao, hamtoki hapa, asipokuja huku huyo ndugu yenu mdogo.
Mwanzo 44:21 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Ukatuambia watumwa wako, Mleteni kwangu, ili macho yangu yamwangalie. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Bwana, ulituagiza sisi watumishi wako kumleta huyo mdogo wetu upate kumwona. Biblia Habari Njema - BHND Bwana, ulituagiza sisi watumishi wako kumleta huyo mdogo wetu upate kumwona. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Bwana, ulituagiza sisi watumishi wako kumleta huyo mdogo wetu upate kumwona. Neno: Bibilia Takatifu “Ndipo ulipowaambia watumishi wako, ‘Mleteni kwangu ili niweze kumwona kwa macho yangu mwenyewe.’ Neno: Maandiko Matakatifu “Ndipo ulipowaambia watumishi wako, ‘Mleteni kwangu ili niweze kumwona kwa macho yangu mwenyewe.’ BIBLIA KISWAHILI Ukatuambia watumwa wako, Mleteni kwangu, ili macho yangu yamwangalie. |
Mtabainika kwa njia hii; aishivyo Farao, hamtoki hapa, asipokuja huku huyo ndugu yenu mdogo.
mkamlete ndugu yenu mdogo kwangu; hivyo maneno yenu yatahakikishwa, wala hamtakufa. Ndivyo walivyofanya.
Akainua macho yake, akamwona Benyamini, nduguye, mwana wa mama yake, akasema, Huyu ndiye ndugu yenu mdogo, mliyeniambia habari zake? Akasema, Mungu akufadhili, mwanangu.
Tukakuambia, bwana wangu, Kijana hawezi kumwacha babaye, maana akimwacha babaye, babaye atakufa.
Kwa maana nitawaelekezea macho yangu, wapate mema, nami nitawaingiza katika nchi hii tena; nami nitawajenga, wala sitawabomoa; nitawapanda wala sitawang'oa.
Na sasa, tazama, nakufungulia leo minyororo hii iliyo mikononi mwako. Kama ukiona ni vema kwenda Babeli pamoja nami, haya! Njoo, nami nitakutunza sana; lakini kama ukiona ni vibaya kwenda Babeli pamoja nami, basi, acha; tazama, nchi yote iko mbele yako; palipo pema machoni pako na pa kukufaa, nenda huko.
Nao wajapokwenda kuwa mateka mbele ya adui zao, nitauagiza upanga huko, nao utawaua; nami nitawaelekezea macho yangu niwatende mabaya, wala si mema.