Kama ninyi ni wa kweli, mmoja wenu na afungwe gerezani, nanyi mwende mkachukue nafaka kwa ajili ya njaa ya nyumba zenu,
Mwanzo 42:26 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Wakawatwika punda wao nafaka yao, wakatoka huko. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wakawatwisha punda wao mizigo yao ya nafaka, wakaondoka. Biblia Habari Njema - BHND Wakawatwisha punda wao mizigo yao ya nafaka, wakaondoka. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wakawatwisha punda wao mizigo yao ya nafaka, wakaondoka. Neno: Bibilia Takatifu wakapakiza nafaka juu ya punda wao, wakaondoka. Neno: Maandiko Matakatifu wakapakiza nafaka juu ya punda zao, wakaondoka. BIBLIA KISWAHILI Wakawatwika punda wao nafaka yao, wakatoka huko. |
Kama ninyi ni wa kweli, mmoja wenu na afungwe gerezani, nanyi mwende mkachukue nafaka kwa ajili ya njaa ya nyumba zenu,
mkamlete ndugu yenu mdogo kwangu; hivyo maneno yenu yatahakikishwa, wala hamtakufa. Ndivyo walivyofanya.
Yusufu akaamuru kuvijaza vyombo vyao nafaka, na kumrudishia kila mtu fedha yake katika gunia lake, na kuwapa chakula cha njiani. Na hivyo ndivyo walivyofanyiwa.
Mmoja wao alipofungua gunia lake ili ampe punda wake chakula katika nyumba ya wageni, aliiona fedha yake; kumbe! Iko kinywani mwa gunia lake.