Baada ya siku tatu Farao atakiinua kichwa chako, atakurudisha katika kazi yako; nawe utampa Farao kikombe mkononi mwake, kama desturi ya kwanza, ulipokuwa mnyweshaji wake.
Mwanzo 40:21 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Akamrudisha mkuu wa wanyweshaji katika kazi yake ya kunywesha, naye akampa Farao kikombe mkononi mwake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kisha akamrudishia cheo chake mtunza vinywaji, apate kumpatia Farao kikombe. Biblia Habari Njema - BHND Kisha akamrudishia cheo chake mtunza vinywaji, apate kumpatia Farao kikombe. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kisha akamrudishia cheo chake mtunza vinywaji, apate kumpatia Farao kikombe. Neno: Bibilia Takatifu Ndipo akamrudisha mnyweshaji mkuu kwenye nafasi yake, ili aweke kikombe mkononi mwa Farao tena. Neno: Maandiko Matakatifu Ndipo akamrudisha mnyweshaji mkuu kwenye nafasi yake, ili aweke kikombe mikononi mwa Farao tena, BIBLIA KISWAHILI Akamrudisha mkuu wa wanyweshaji katika kazi yake ya kunywesha, naye akampa Farao kikombe mkononi mwake. |
Baada ya siku tatu Farao atakiinua kichwa chako, atakurudisha katika kazi yako; nawe utampa Farao kikombe mkononi mwake, kama desturi ya kwanza, ulipokuwa mnyweshaji wake.
Ikawa, kama vile alivyotufasiria ndivyo ilivyotokea; mimi nilirudishwa katika kazi yangu, na yeye alitundikwa.
Ee Bwana, nakusihi, litege sikio lako, uyasikilize maombi ya mtumishi wako, na maombi ya watumishi wako, wanaofurahi kulicha jina lako; nakuomba sana; unifanikishe mimi, mtumishi wako, leo, ukanijalie rehema mbele ya mtu huyu. (Maana, nilikuwa mnyweshaji wa mfalme).
Ikawa katika mwezi wa Nisani, mwaka wa ishirini wa mfalme Artashasta, na divai imewekwa mbele yake, nikaishika ile divai, nikampa mfalme. Nami mpaka sasa sikuwa na huzuni mbele ya mfalme wakati wowote.