Mwanzo 40:18 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Yusufu akajibu, akasema, Tafsiri yake ndiyo hii Nyungo tatu ni siku tatu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Yosefu akamwambia, “Tafsiri ya ndoto yako ni hii: Zile nyungo tatu ni siku tatu. Biblia Habari Njema - BHND Yosefu akamwambia, “Tafsiri ya ndoto yako ni hii: Zile nyungo tatu ni siku tatu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Yosefu akamwambia, “Tafsiri ya ndoto yako ni hii: zile nyungo tatu ni siku tatu. Neno: Bibilia Takatifu Yusufu akamwambia, “Hii ndiyo maana yake: Vikapu vitatu ni siku tatu. Neno: Maandiko Matakatifu Yusufu akamwambia, “Hii ndiyo maana yake: Vikapu vitatu ni siku tatu. BIBLIA KISWAHILI Yusufu akajibu, akasema, Tafsiri yake ndiyo hii Nyungo tatu ni siku tatu. |
Na katika ungo wa juu, mlikuwa na kila namna ya chakula kwa Farao, kazi za mwokaji; ndege wakavila katika ungo juu ya kichwa changu.
Baada ya siku tatu Farao atakiinua na kukuondolea kichwa chako, na kukutundika juu ya mti, na ndege watakula nyama yako.
Na huko pamoja nasi palikuwa na kijana; Mwebrania, mtumishi wa mkuu wa askari, tukamhadithia, naye akatufasiria ndoto zetu; akamfasiria kila mtu kama ilivyokuwa ndoto yake.
Wale ng'ombe saba wema ni miaka saba; na yale masuke saba mema ni miaka saba. Ndoto ni moja.
wote wakanywa kinywaji kile kile cha roho; kwa maana waliunywea mwamba wa roho uliowafuata; na mwamba ule ulikuwa ni Kristo.
naye akiisha kushukuru akaumega, akasema, Huu ndio mwili wangu ulio kwa ajili yenu; fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu.