Kwa sababu hakika niliibwa kutoka nchi ya Waebrania, wala hapa sikutenda jambo lolote hata wanitie gerezani.
Mwanzo 39:20 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Bwana wake akamtwaa Yusufu, akamtia gerezani, mahali wafungwa wa mfalme walimokuwa wamefungiwa, naye akawa humo gerezani. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema akamchukua Yosefu na kumtia gerezani, mahali walipofungwa wahalifu wa mfalme. Biblia Habari Njema - BHND akamchukua Yosefu na kumtia gerezani, mahali walipofungwa wahalifu wa mfalme. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza akamchukua Yosefu na kumtia gerezani, mahali walipofungwa wahalifu wa mfalme. Neno: Bibilia Takatifu Potifa akamchukua Yusufu na kumtia gerezani, mahali wahalifu wa mfalme walipokuwa wamefungwa. Lakini Yusufu alipokuwa huko gerezani, Neno: Maandiko Matakatifu Potifa akamchukua Yusufu na kumweka gerezani, mahali ambapo wahalifu wa mfalme walikuwa wamefungwa. Lakini wakati Yusufu alipokuwa huko gerezani, BIBLIA KISWAHILI Bwana wake akamtwaa Yusufu, akamtia gerezani, mahali wafungwa wa mfalme walimokuwa wamefungiwa, naye akawa humo gerezani. |
Kwa sababu hakika niliibwa kutoka nchi ya Waebrania, wala hapa sikutenda jambo lolote hata wanitie gerezani.
Kwa kuonewa na kuhukumiwa aliondolewa; Na maisha yake ni nani angeyajali? Maana amekatiliwa mbali na nchi ya walio hai; Alipigwa kwa sababu ya makosa ya watu wangu.
Nao wakuu wakamkasirikia Yeremia, wakampiga, wakamtia gerezani katika nyumba ya Yonathani, mwandishi; kwa maana ndiyo waliyoifanya kuwa gereza.
Nami katika hiyo nimeteswa hata kufungwa kama mtenda mabaya; lakini neno la Mungu halifungwi.
wengine walijaribiwa kwa dhihaka na mapigo, naam, kwa minyororo, na kwa kutiwa gerezani;
Maana huu ndio wema hasa, mtu akivumilia huzuni kwa kumkumbuka Mungu, pale ateswapo pasipo haki.