Mwanzo 39:19 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Ikawa bwana wake aliposikia maneno aliyoambia na mkewe, akisema, Mtumwa wako amenitendea mambo kama haya, hasira yake ikawaka. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Basi, bwana wake Yosefu alipoyasikia maneno ya mkewe, kwamba ndivyo mtumishi wake alivyomtendea, akawaka hasira, Biblia Habari Njema - BHND Basi, bwana wake Yosefu alipoyasikia maneno ya mkewe, kwamba ndivyo mtumishi wake alivyomtendea, akawaka hasira, Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Basi, bwana wake Yosefu alipoyasikia maneno ya mkewe, kwamba ndivyo mtumishi wake alivyomtendea, akawaka hasira, Neno: Bibilia Takatifu Potifa aliposikia kisa alichosimuliwa na mkewe, akisema, “Hivi ndivyo mtumwa wako alivyonitenda,” hasira yake ikawaka. Neno: Maandiko Matakatifu Potifa aliposikia kisa hiki mkewe alichomweleza, akisema, “Hivi ndivyo mtumwa wako alivyonitenda.” Hasira ya Potifa ikawaka. BIBLIA KISWAHILI Ikawa bwana wake aliposikia maneno aliyoambia na mkewe, akisema, Mtumwa wako amenitendea mambo kama haya, hasira yake ikawaka. |
Maji mengi hayawezi kuuzimisha upendo, Wala mito haiwezi kuuzamisha; Kama mtu angetoa badala ya upendo Mali yote ya nyumbani mwake, Angedharauliwa kabisa.
Nikawajibu kwamba si desturi ya Warumi kumtoa mtu awaye yote, kabla mtu yule aliyeshitakiwa hajaonana na washitaki wake uso kwa uso, na kupewa nafasi ya kujitetea katika mashitaka yake.