Basi akavua nguo za ujane wake, akajivika utaji, akajifunika uso, akakaa mlangoni pa Enaimu, karibu na njia ya kuendea Timna. Maana aliona ya kwamba Shela amekuwa mtu mzima, ijapokuwa hakuozwa awe mkewe.
Mwanzo 38:19 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Akaondoka, akaenda zake, akavua utaji wake, na kuvaa mavazi ya ujane wake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Basi, Tamari akarudi nyumbani akavua ile shela aliyojifunika, akavaa tena mavazi yake ya ujane. Biblia Habari Njema - BHND Basi, Tamari akarudi nyumbani akavua ile shela aliyojifunika, akavaa tena mavazi yake ya ujane. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Basi, Tamari akarudi nyumbani akavua ile shela aliyojifunika, akavaa tena mavazi yake ya ujane. Neno: Bibilia Takatifu Tamari akaondoka, akavua shela yake, akavaa tena nguo zake za ujane. Neno: Maandiko Matakatifu Tamari akaondoka, akavua shela yake akavaa tena nguo zake za ujane. BIBLIA KISWAHILI Akaondoka, akaenda zake, akavua utaji wake, na kuvaa mavazi ya ujane wake. |
Basi akavua nguo za ujane wake, akajivika utaji, akajifunika uso, akakaa mlangoni pa Enaimu, karibu na njia ya kuendea Timna. Maana aliona ya kwamba Shela amekuwa mtu mzima, ijapokuwa hakuozwa awe mkewe.
Akasema, Nikupe rehani gani? Akamjibu, Pete yako ya mhuri, na kamba yake, na fimbo yako iliyo mkononi mwako. Basi akampa, akaingia kwake, naye akapata mimba.
Yuda akapeleka yule mwana-mbuzi kwa mkono wa rafiki yake Mwadulami, ili aipate rehani mkononi mwa huyo mwanamke lakini hakumkuta.
Yoabu akatuma watu waende Tekoa, akaleta kutoka huko mwanamke mwenye akili, akamwambia, Nakusihi, ujifanye kama unaomboleza, ukavae nguo za kufiwa, nakusihi, wala usijitie mafuta, ila ukafanane na mwanamke aliyeomboleza siku nyingi kwa ajili yake aliyefariki;
Mfalme akamwuliza, Una nini? Naye akajibu, Hakika ni mjane mimi, niliyefiwa na mume wangu.