Esau akamchukia Yakobo kwa ajili ya ile baraka babaye aliyombariki. Esau akasema moyoni mwake, Siku za kumlilia baba yangu zinakaribia, ndipo nitakapomwua ndugu yangu Yakobo.
Mwanzo 37:4 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Ndugu zake wakaona ya kuwa baba yao anampenda kuliko ndugu zake wote, wakamchukia, wala hawakuweza kusema naye kwa amani. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Lakini ndugu zake walipoona kwamba baba yao alimpenda Yosefu kuliko wao, wakamchukia hata hawakuzungumza naye kwa amani. Biblia Habari Njema - BHND Lakini ndugu zake walipoona kwamba baba yao alimpenda Yosefu kuliko wao, wakamchukia hata hawakuzungumza naye kwa amani. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Lakini ndugu zake walipoona kwamba baba yao alimpenda Yosefu kuliko wao, wakamchukia hata hawakuzungumza naye kwa amani. Neno: Bibilia Takatifu Ndugu zake walipoona kwamba baba yao anampenda Yusufu kuliko yeyote kati yao, walimchukia na hawakusema naye neno lolote jema. Neno: Maandiko Matakatifu Ndugu zake walipoona kwamba baba yao anampenda Yusufu kuliko yeyote mwingine miongoni mwao, walimchukia na hawakusema naye neno lolote jema. BIBLIA KISWAHILI Ndugu zake wakaona ya kuwa baba yao anampenda kuliko ndugu zake wote, wakamchukia, wala hawakuweza kusema naye kwa amani. |
Esau akamchukia Yakobo kwa ajili ya ile baraka babaye aliyombariki. Esau akasema moyoni mwake, Siku za kumlilia baba yangu zinakaribia, ndipo nitakapomwua ndugu yangu Yakobo.
bali Kaini hakumtakabali, wala sadaka yake. Kaini akaghadhibika sana, uso wake ukakunjamana.
Wanaonichukia bure ni wengi Kuliko nywele za kichwa changu. Watakao kunikatilia mbali ni wengi, Adui zangu kwa sababu isiyo kweli. Hata mimi nililipishwa kwa nguvu Vitu nisivyovichukua.
Kwa maana hata ndugu zako, na nyumba ya baba yako, wamekutenda mambo ya hila; naam, wamepiga kelele nyuma yako; usiwasadiki, wajapokuambia maneno mazuri.
Maana hapo zamani sisi nasi tulikuwa hatuna akili, tulikuwa waasi, tumedanganywa, huku tukitumikia tamaa na anasa za namna nyingi, tukiishi katika uovu na husuda, tukichukiza na kuchukiana.
Bali yeye amchukiaye ndugu yake, yuko katika giza, tena anakwenda katika giza, wala hajui aendako, kwa sababu giza imempofusha macho.
Katika hili watoto wa Mungu ni dhahiri, na watoto wa Ibilisi nao. Mtu yeyote asiyetenda haki hatokani na Mungu, wala yeye asiyempenda ndugu yake.
si kama Kaini alivyokuwa wa yule mwovu, akamwua ndugu yake. Naye alimwua kwa sababu gani? Kwa sababu matendo yake yalikuwa mabaya, na ya ndugu yake yalikuwa ya haki.
Mtu akisema, Nampenda Mungu, naye anamchukia ndugu yake, ni mwongo; kwa maana asiyempenda ndugu yake ambaye amemwona, hawezi kumpenda Mungu ambaye hakumwona.
Naye Eliabu, mkubwa wake, alisikia hapo alipoongea na watu; na hasira yake Eliabu ikawaka juu ya Daudi, akasema, Mbona wewe umeshuka hapa? Na kondoo wale wachache umemwachia nani kule nyikani? Mimi nakujua kiburi chako, na ubaya wa moyo wako; maana umeshuka ili upate kuvitazama vita.