Ikawa Yusufu alipofika kwa ndugu zake, wakamvua Yusufu kanzu yake, kanzu ile ndefu aliyoivaa,
Mwanzo 37:24 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC wakamtwaa wakamtupa katika shimo; na hilo shimo ilikuwa tupu, hamna maji. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kisha wakamshika na kumtupa shimoni. Lakini shimo hilo halikuwa na maji. Biblia Habari Njema - BHND Kisha wakamshika na kumtupa shimoni. Lakini shimo hilo halikuwa na maji. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kisha wakamshika na kumtupa shimoni. Lakini shimo hilo halikuwa na maji. Neno: Bibilia Takatifu Kisha wakamchukua, wakamtupa katika shimo. Hilo shimo lilikuwa tupu, halikuwa na maji. Neno: Maandiko Matakatifu Kisha wakamchukua wakamtupa katika shimo. Wakati huo shimo lilikuwa tupu, halikuwa na maji ndani yake. BIBLIA KISWAHILI wakamtwaa wakamtupa katika shimo; na hilo shimo ilikuwa tupu, hamna maji. |
Ikawa Yusufu alipofika kwa ndugu zake, wakamvua Yusufu kanzu yake, kanzu ile ndefu aliyoivaa,
Nao wakakaa kitako kula chakula; wakainua macho yao, wakaona, msafara wa Waishmaeli wanakuja wakitoka Gileadi na ngamia zao, wakichukua ubani na zeri na manemane, wakisafiri kuvichukua mpaka Misri.
Wakaambiana, Kweli sisi tulimkosea ndugu yetu, kwa kuwa tuliona shida ya roho yake, alipotusihi, wala hatukusikia, kwa hiyo shida hii imetupata.
Akanipandisha toka shimo la uharibifu, Toka udongo wa utelezi; Akaisimamisha miguu yangu mwambani, Akaziimarisha hatua zangu.
Basi wakamtwaa Yeremia, wakamtupa katika shimo la Malkiya, mwana wa mfalme, lililo katika ukumbi wa walinzi; wakamshusha kwa kamba. Na mle shimoni hamkuwa na maji, ila matope tu; naye Yeremia akazama katika matope hayo.
Pumzi ya mianzi ya pua zetu, masihi wa BWANA, Alikamatwa katika marima yao; Ambaye kwa habari zake tulisema, Chini ya kivuli chake tutakaa kati ya mataifa.
Na kwa habari zako wewe, kwa sababu ya damu ya agano lako, nimewatoa wafungwa wako katika shimo lile lisilo na maji.