Reubeni akawaambia, Msimwage damu; mtupeni katika shimo hili lililopo nyikani, wala msimguse; ili apate kumwokoa katika mikono yao, akamrudishe kwa baba yake.
Mwanzo 37:23 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Ikawa Yusufu alipofika kwa ndugu zake, wakamvua Yusufu kanzu yake, kanzu ile ndefu aliyoivaa, Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Yosefu alipowafikia ndugu zake, wao wakamvua kanzu yake. Biblia Habari Njema - BHND Yosefu alipowafikia ndugu zake, wao wakamvua kanzu yake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Yosefu alipowafikia ndugu zake, wao wakamvua kanzu yake. Neno: Bibilia Takatifu Kwa hiyo Yusufu alipowafikia ndugu zake, walimvua lile joho lake, lile joho lililofumwa vizuri alilokuwa amevaa. Neno: Maandiko Matakatifu Kwa hiyo Yusufu alipowafikia ndugu zake, walimvua lile joho lake, lile joho lililorembwa vizuri alilokuwa amevaa. BIBLIA KISWAHILI Ikawa Yusufu alipofika kwa ndugu zake, wakamvua Yusufu kanzu yake, kanzu ile ndefu aliyoivaa, |
Reubeni akawaambia, Msimwage damu; mtupeni katika shimo hili lililopo nyikani, wala msimguse; ili apate kumwokoa katika mikono yao, akamrudishe kwa baba yake.
Basi Israeli akampenda Yusufu kuliko wanawe wote, maana ni mwana wa uzee wake, akamfanyia kanzu ndefu.
Wakaambiana, Kweli sisi tulimkosea ndugu yetu, kwa kuwa tuliona shida ya roho yake, alipotusihi, wala hatukusikia, kwa hiyo shida hii imetupata.
Naye alikuwa amevaa kanzu ndefu; kwa kuwa kwa nguo hizo huvikwa binti za mfalme waliokuwa wanawali. Ndipo mtumishi wake akamtoa nje, akafunga mlango nyuma yake.