Na hawa ni wana wa Oholibama, binti Ana, binti Sibeoni, mkewe Esau; akamzalia Esau, Yeushi, na Yalamu, na Kora.
Mwanzo 36:15 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Hawa ndio majumbe wao wana wa Esau; wana wa Elifazi, mzaliwa wa kwanza wa Esau; jumbe Temani, jumbe Omari, jumbe Sefo, jumbe Kenazi, Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wafuatao ni wakuu wa makabila yaliyotokana na Esau. Elifazi, aliyekuwa mzaliwa wa kwanza wa Esau aliwazaa Temani, Omari, Sefo, Kenazi, Biblia Habari Njema - BHND Wafuatao ni wakuu wa makabila yaliyotokana na Esau. Elifazi, aliyekuwa mzaliwa wa kwanza wa Esau aliwazaa Temani, Omari, Sefo, Kenazi, Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wafuatao ni wakuu wa makabila yaliyotokana na Esau. Elifazi, aliyekuwa mzaliwa wa kwanza wa Esau aliwazaa Temani, Omari, Sefo, Kenazi, Neno: Bibilia Takatifu Hawa walikuwa wakuu miongoni mwa wazao wa Esau: Wakuu wa wana wa Elifazi, mzaliwa wa kwanza wa Esau ni: Temani, Omari, Sefo, Kenazi, Neno: Maandiko Matakatifu Hawa ndio waliokuwa wakuu miongoni mwa wazao wa Esau: Wakuu wa wana wa Elifazi, mzaliwa wa kwanza wa Esau ni: Temani, Omari, Sefo, Kenazi, BIBLIA KISWAHILI Hawa ndio majumbe wao wana wa Esau; wana wa Elifazi, mzaliwa wa kwanza wa Esau; jumbe Temani, jumbe Omari, jumbe Sefo, jumbe Kenazi, |
Na hawa ni wana wa Oholibama, binti Ana, binti Sibeoni, mkewe Esau; akamzalia Esau, Yeushi, na Yalamu, na Kora.
jumbe Kora, jumbe Gatamu, jumbe Amaleki. Hao ndio majumbe, waliotoka kwa Elifazi katika nchi ya Edomu. Hao ni wana wa Ada.
Na hawa ni wana wa Oholibama, mkewe Esau; jumbe Yeushi, jumbe Yalamu, jumbe Kora. Hao ndio majumbe waliotoka kwa Oholibama, binti Ana, mkewe Esau.
Basi ikawa hao marafiki watatu wa Ayubu walipopata habari ya mabaya hayo yote yaliyomfikia, wakaja kila mtu kutoka mahali pake; nao ni Elifazi Mtemani, na Bildadi Mshuhi, na Sofari Mnaamathi; wakapatana pamoja ili waende kumfariji Ayubu na kumtuliza moyo.
Ndipo majumbe wa Edomu wakashangaa, Watu wa Moabu wenye nguvu tetemeko limewapata, Watu wote wakaao Kanaani wameyeyuka.
Basi, lisikieni shauri la BWANA; Alilolifanya juu ya Edomu; Na makusudi yake aliyoyakusudia Juu yao wakaao Temani; Hakika watawaburura, naam, wadogo wa kundi; Hakika malisho yao yatafadhaika kwa ajili yao.
Kuhusu Edomu. BWANA wa majeshi asema hivi, Je! Hakuna tena hekima katika Temani? Mashauri yamewapotea wenye busara? Je! Imetoweka hekima yao?
kwa sababu hiyo, Bwana MUNGU asema hivi; Nitanyosha mkono wangu juu ya Edomu, nitakatilia mbali nayo wanadamu na wanyama; nami nitaifanya kuwa ukiwa toka Temani; na mpaka Dedani wataanguka kwa upanga.
Na mashujaa wako, Ee Temani, watafadhaika, hata iwe kila mtu akatiliwe mbali kwa kuuawa katika kilima cha Esau.
Mungu alikuja kutoka Temani, Yeye aliye mtakatifu kutoka mlima Parani. Utukufu wake ukazifunika mbingu, Nayo dunia ikajaa sifa yake.