Kisha wakarudi wakaja mpaka Enmisfati, ndio Kadeshi, wakapiga nchi yote ya Waamaleki, na Waamori waliokaa Hasason-tamari.
Mwanzo 36:12 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Na Timna alikuwa suria wa Elifazi, mwana wa Esau; naye akamzalia Elifazi Amaleki. Hao ndio wana wa Ada, mkewe Esau. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Elifazi alikuwa na suria jina lake Timna. Huyu alimzalia mwana, jina lake Amaleki. Biblia Habari Njema - BHND Elifazi alikuwa na suria jina lake Timna. Huyu alimzalia mwana, jina lake Amaleki. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Elifazi alikuwa na suria jina lake Timna. Huyu alimzalia mwana, jina lake Amaleki. Neno: Bibilia Takatifu Elifazi mwana wa Esau alikuwa pia na suria aliyeitwa Timna, aliyemzalia Amaleki. Hao walikuwa wajukuu wa Ada mke wa Esau. Neno: Maandiko Matakatifu Elifazi mwana wa Esau alikuwa pia na suria aliyeitwa Timna, ambaye alimzalia Amaleki. Hawa ndio waliokuwa wajukuu wa Ada mke wa Esau. BIBLIA KISWAHILI Na Timna alikuwa suria wa Elifazi, mwana wa Esau; naye akamzalia Elifazi Amaleki. Hao ndio wana wa Ada, mkewe Esau. |
Kisha wakarudi wakaja mpaka Enmisfati, ndio Kadeshi, wakapiga nchi yote ya Waamaleki, na Waamori waliokaa Hasason-tamari.
Na hawa ni wana wa Reueli: Nahathi, na Zera, na Shama na Miza. Hao walikuwa wana wa Basemathi, mkewe Esau.
Wana wa Elifazi; Temani, na Omari, na Sefo, na Gatamu, na Kenazi, na, kwa Timna, Amaleki.
Usimchukie Mwedomi; kwa kuwa ni ndugu yako; usimchukie Mmisri, kwa kuwa ulikuwa mgeni katika nchi yake.