Mwanzo 35:25 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Wana wa Bilha, kijakazi wa Raheli, ni Dani na Naftali. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Watoto wa kiume waliozaliwa na Bilha, mjakazi wa Raheli, walikuwa Dani na Naftali. Biblia Habari Njema - BHND Watoto wa kiume waliozaliwa na Bilha, mjakazi wa Raheli, walikuwa Dani na Naftali. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Watoto wa kiume waliozaliwa na Bilha, mjakazi wa Raheli, walikuwa Dani na Naftali. Neno: Bibilia Takatifu Wana waliozaliwa na Bilha mjakazi wa Raheli walikuwa: Dani na Naftali. Neno: Maandiko Matakatifu Wana waliozaliwa na Bilha mtumishi wa kike wa Raheli walikuwa: Dani na Naftali. BIBLIA KISWAHILI Wana wa Bilha, kijakazi wa Raheli, ni Dani na Naftali. |
Hivi ndivyo vizazi vya Yakobo. Yusufu, aliyekuwa mwenye miaka kumi na saba, alikuwa akichunga kondoo pamoja na ndugu zake; naye alikuwa kijana pamoja na wana wa Bilha, na wana wa Zilpa, wake wa baba yake. Yusufu akamletea baba yao habari zao mbaya.
Kisha sehemu ya sita ikatokea kwa ajili ya wana wa Naftali, maana, ni kwa ajili ya wana wa Naftali kwa kufuata jamaa zao.
Kisha sehemu ya saba ilitokea kwa ajili ya kabila la wana wa Dani kwa kufuata jamaa zao.
Gileadi alikaa ng'ambo ya Yordani, Na Dani, mbona alikaa katika merikebu? Asheri alikaa kimya penye bandari ya bahari, Alikaa katika hori zake.
Zabuloni ndio watu waliohatarisha roho zao hadi kufa; Nao Naftali mahali palipoinuka kondeni.