Lakini Benyamini, ndugu wa Yusufu, Yakobo hakumpeleka pamoja na ndugu zake, maana alisema, Mabaya yasimpate.
Mwanzo 35:24 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Wana wa Raheli, ni Yusufu na Benyamini. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Watoto wa kiume wa Raheli walikuwa Yosefu na Benyamini. Biblia Habari Njema - BHND Watoto wa kiume wa Raheli walikuwa Yosefu na Benyamini. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Watoto wa kiume wa Raheli walikuwa Yosefu na Benyamini. Neno: Bibilia Takatifu Wana wa Raheli walikuwa: Yusufu na Benyamini. Neno: Maandiko Matakatifu Wana wa Raheli walikuwa: Yusufu na Benyamini. BIBLIA KISWAHILI Wana wa Raheli, ni Yusufu na Benyamini. |
Lakini Benyamini, ndugu wa Yusufu, Yakobo hakumpeleka pamoja na ndugu zake, maana alisema, Mabaya yasimpate.
Akainua macho yake, akamwona Benyamini, nduguye, mwana wa mama yake, akasema, Huyu ndiye ndugu yenu mdogo, mliyeniambia habari zake? Akasema, Mungu akufadhili, mwanangu.
Wakapelekewa sehemu za chakula kutoka mezani pake, lakini akazidisha sehemu ya Benyamini iwe kubwa mara tano kuliko zao. Wakanywa, wakafurahi pamoja naye.
Sehemu waliopewa wana wa Yusufu ilianza kutoka mto wa Yordani hapo Yeriko, hapo penye maji ya Yeriko upande wa mashariki, maana, ni hiyo nyika, kukwea kutoka Yeriko kati ya hiyo nchi ya vilima mpaka Betheli;
Kisha ilizuka kura ya kabila la wana wa Benyamini kwa kulingana na jamaa zao; na mpaka wa hiyo kura yao ukatokea kati ya wana wa Yuda na wana wa Yusufu.
Kutoka Efraimu waliteremka wao ambao shina lao ni katika Amaleki, Nyuma yako, Benyamini, kati ya watu wako. Kutoka Makiri walishuka makamanda, Na kutoka Zabuloni wao washikao fimbo ya mwandishi.
Na watu wote waliokuwapo langoni, na wale wazee, wakasema, Naam, sisi ni mashahidi. BWANA na amfanye mwanamke huyu aingiaye nyumbani mwako kuwa kama Raheli na kama Lea, wale wawili walioijenga nyumba ya Israeli. Nawe ufanikiwe katika Efrata, na kuwa mashuhuri katika Bethlehemu.