Wakasafiri kutoka Betheli, na kabla ya kufika Efrata, Raheli akashikwa na uchungu wa kuzaa, na uchungu wake ulikuwa mkali.
Mwanzo 35:19 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Akafa Raheli, akazikwa katika njia ya Efrata, ndio Bethlehemu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Basi, Raheli akafariki na kuzikwa kando ya njia iendayo Efratha (yaani Bethlehemu). Biblia Habari Njema - BHND Basi, Raheli akafariki na kuzikwa kando ya njia iendayo Efratha (yaani Bethlehemu). Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Basi, Raheli akafariki na kuzikwa kando ya njia iendayo Efratha (yaani Bethlehemu). Neno: Bibilia Takatifu Kwa hiyo Raheli akafa, na akazikwa kando ya njia iendayo Efrata (ndio Bethlehemu). Neno: Maandiko Matakatifu Kwa hiyo Raheli akafa, akazikwa kando ya njia iendayo Efrathi (ndio Bethlehemu). BIBLIA KISWAHILI Akafa Raheli, akazikwa katika njia ya Efrata, ndio Bethlehemu. |
Wakasafiri kutoka Betheli, na kabla ya kufika Efrata, Raheli akashikwa na uchungu wa kuzaa, na uchungu wake ulikuwa mkali.
Ikawa hapo katika kutoa roho yake, maana alikufa, akamwita jina lake Benoni, lakini babaye alimwita Benyamini.
Na mimi nilipokuja kutoka Padan, Raheli akanifia katika nchi ya Kanaani, njiani, si mwendo mkubwa kabla ya kufika Efrata. Nikamzika katika njia ya Efrata, ndio Bethlehemu.
Naye Daudi wakati ule alikuwako ngomeni, na jeshi la Wafilisti wakati ule walikuwako Bethlehemu.
Daudi akatamani, akasema, Laiti mtu angeninywesha maji ya kisima cha Bethlehemu, kilicho karibu na lango!
Sasa utajikusanya vikosi vikosi, Ee binti wa vikosi; yeye amemhusuru; watampiga mwamuzi wa Israeli shavuni mwake kwa fimbo.
Bali wewe, Bethlehemu Efrata, uliye mdogo kuwa miongoni mwa elfu za Yuda; kutoka kwako wewe atanitokea mmoja atakayekuwa mtawala katika Israeli; ambaye asili yake imekuwa tangu zamani za kale, tangu milele.
Sikieni, enyi milima, shutuma ya BWANA, na ninyi, enyi misingi ya dunia iliyo imara; kwa maana BWANA ana shutuma na watu wake, naye atahojiana na Israeli.
Yesu alipozaliwa katika Bethlehemu ya Uyahudi zamani za mfalme Herode, tazama, majusi wa mashariki walifika Yerusalemu, wakisema,
Nawe Bethlehemu, katika nchi ya Yuda, Hu mdogo kamwe miongoni mwa watawala wa Yuda; Kwa kuwa kwako atatoka mtawala Atakayewachunga watu wangu Israeli.
Katathi, Nahalali, Shimroni, Idala na Bethlehemu; miji kumi na miwili, pamoja na vijiji vyake.
Alikuwako mtu kijana mmoja mwanamume aliyetoka Bethlehemu-yuda, wa jamaa ya Yuda, aliyekuwa Mlawi, naye akakaa huko kama mgeni.
Na jina la mtu huyo aliitwa Elimeleki, na jina la mkewe Naomi, na majina ya wanawe wawili Maloni na Kilioni, Waefrata wa Bethlehemu ya Yuda. Wakafika nchi ya Moabu, wakakaa huko.
Na watu wote waliokuwapo langoni, na wale wazee, wakasema, Naam, sisi ni mashahidi. BWANA na amfanye mwanamke huyu aingiaye nyumbani mwako kuwa kama Raheli na kama Lea, wale wawili walioijenga nyumba ya Israeli. Nawe ufanikiwe katika Efrata, na kuwa mashuhuri katika Bethlehemu.
Utakapoondoka kwangu leo, utakutana na wanaume wawili karibu na kaburi la Raheli, katika mpaka wa Benyamini huko Selsa; nao watakuambia, Punda hao uliokwenda kuwatafuta wameonekana; na tazama, baba yako ameacha kufikiri habari za punda, anafikiri habari zenu, akisema, Nifanye nini kwa ajili ya mwanangu?
Samweli akafanya hayo aliyosema BWANA, akaenda Bethlehemu. Wakaja wazee wa mji kumlaki, wakitetemeka, nao wakasema, Je! Umekuja kwa amani?
Basi Daudi alikuwa mwana wa yule Mwefrata, wa Bethlehemu ya Yuda, aliyeitwa jina lake Yese; naye huyo alikuwa na wana wanane; na yeye mwenyewe alikuwa mzee siku za Sauli, na mkongwe miongoni mwa watu.