Basi Yakobo akasikia ya kwamba amembikiri Dina, binti yake. Na wanawe walikuwako pamoja na wanyama wake nyikani. Yakobo akanyamaza, hadi walipokuja.
Mwanzo 34:6 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Akatoka Hamori, babaye Shekemu, kumwendea Yakobo, aseme naye. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hamori, baba yake Shekemu, akaenda kwa Yakobo ili azungumze naye, Biblia Habari Njema - BHND Hamori, baba yake Shekemu, akaenda kwa Yakobo ili azungumze naye, Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hamori, baba yake Shekemu, akaenda kwa Yakobo ili azungumze naye, Neno: Bibilia Takatifu Kisha Hamori baba yake Shekemu akaenda kuzungumza na Yakobo. Neno: Maandiko Matakatifu Kisha Hamori baba yake Shekemu akaenda kuzungumza na Yakobo. BIBLIA KISWAHILI Akatoka Hamori, babaye Shekemu, kumwendea Yakobo, aseme naye. |
Basi Yakobo akasikia ya kwamba amembikiri Dina, binti yake. Na wanawe walikuwako pamoja na wanyama wake nyikani. Yakobo akanyamaza, hadi walipokuja.
Wanawe Yakobo waliposikia hayo, wakaja kutoka malishoni; nao wakasikitika sana, wakakasirika mno, kwa sababu amefanya upumbavu katika Israeli kwa kulala na binti Yakobo, jambo lisilostahili kutendeka.
Naye Gaali mwana wa Ebedi akasema, Abimeleki ni nani, na sisi wa Shekemu ni nani, hata tukamtumikie yeye? Je, huyu mwana wa Yerubaali na Zebuli afisa wake hawakuwatumikia watu wa Hamori babaye Shekemu? Basi, kwa nini tumutumikie?