Wana wa Yakobo wakawajibu Shekemu na Hamori babaye, kwa hila, maana amemharibu Dina, dada yao,
Mwanzo 34:31 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Nao wakasema, Je! Ni vema amtendee dada yetu kama kahaba? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hao ndugu wawili wakajibu, “Ana haki gani ya kumtendea dada yetu kama malaya?” Biblia Habari Njema - BHND Hao ndugu wawili wakajibu, “Ana haki gani ya kumtendea dada yetu kama malaya?” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hao ndugu wawili wakajibu, “Ana haki gani ya kumtendea dada yetu kama malaya?” Neno: Bibilia Takatifu Lakini wakamjibu, “Je, ilikuwa vyema kumtendea dada yetu kama kahaba?” Neno: Maandiko Matakatifu Lakini wakamjibu, “Je, ilikuwa vyema kumtendea dada yetu kama kahaba?” BIBLIA KISWAHILI Nao wakasema, Je! Ni vema amtendee dada yetu kama kahaba? |
Wana wa Yakobo wakawajibu Shekemu na Hamori babaye, kwa hila, maana amemharibu Dina, dada yao,
Yakobo akawaambia Simeoni na Lawi, Mmenitaabisha, kunifanya ninuke vibaya kati ya watu wa nchi hii, Wakanaani na Waperizi; na mimi, kwa kuwa watu wangu ni haba, watanikusanyikia, na kunipiga, nami nitaangamizwa, mimi na nyumba yangu.
Mungu akamwambia Yakobo, Ondoka, panda uende Betheli, ukakae huko; ukamfanyie Mungu madhabahu huko; yeye aliyekutokea ulipomkimbia Esau, ndugu yako.
Ghadhabu yao na ilaaniwe, maana ilikuwa kali, Na hasira yao, maana ilikuwa haina huruma. Nitawagawa katika Yakobo, Nitawatawanya katika Israeli.