Labani akamwambia Yakobo, Umefanya nini? Umenihadaa, ukawachukua binti zangu kama mateka waliotwaliwa kwa upanga.
Mwanzo 34:29 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Wakatwaa na mali yao zote, watoto wao wote, na wake zao wakateka na hata wakapora vyote vilivyokuwemo nyumbani. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Waliteka nyara mali yote, watoto na wanawake wote na chochote kilichokuwa majumbani. Biblia Habari Njema - BHND Waliteka nyara mali yote, watoto na wanawake wote na chochote kilichokuwa majumbani. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Waliteka nyara mali yote, watoto na wanawake wote na chochote kilichokuwa majumbani. Neno: Bibilia Takatifu Waliteka utajiri wao wote, pamoja na wanawake na watoto wao, wakapora kila kitu ndani ya nyumba zao. Neno: Maandiko Matakatifu Walichukua utajiri wao wote pamoja na wanawake na watoto wao, wakachukua nyara kila kitu ndani ya nyumba zao. BIBLIA KISWAHILI Wakatwaa na mali zao zote, watoto wao wote, na wake zao wakateka na hata wakapora vyote vilivyokuwemo nyumbani. |
Labani akamwambia Yakobo, Umefanya nini? Umenihadaa, ukawachukua binti zangu kama mateka waliotwaliwa kwa upanga.
Wakachukua kondoo wao, na ng'ombe wao, na punda wao, na vitu vilivyokuwamo mjini, na vile vilivyokuwako kondeni.
Yakobo akawaambia Simeoni na Lawi, Mmenitaabisha, kunifanya ninuke vibaya kati ya watu wa nchi hii, Wakanaani na Waperizi; na mimi, kwa kuwa watu wangu ni haba, watanikusanyikia, na kunipiga, nami nitaangamizwa, mimi na nyumba yangu.
Wana wa Israeli wakawachukua mateka wanawake wa Midiani na watoto wao; na ng'ombe zao wote, na kondoo zao wote, na mali zao zote, wakachukua nyara.