Lakini kwa sharti hiyo moja tu watapatana nasi wakae wote kwetu, tuwe watu wamoja, kama tukitahiriwa kila mwanamume, kama wao walivyotahiriwa.
Mwanzo 34:23 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Je! Kondoo zao, na mali zao, na wanyama wao wote hawatakuwa mali zetu? Basi na tupatane nao tu, nao watakaa kwetu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Je, hamwoni kwamba mifugo yao na mali yao yote itakuwa mali yetu? Haya, tukubaliane nao ili wakae pamoja nasi.” Biblia Habari Njema - BHND Je, hamwoni kwamba mifugo yao na mali yao yote itakuwa mali yetu? Haya, tukubaliane nao ili wakae pamoja nasi.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Je, hamwoni kwamba mifugo yao na mali yao yote itakuwa mali yetu? Haya, tukubaliane nao ili wakae pamoja nasi.” Neno: Bibilia Takatifu Je, si mifugo yao, mali yao na wanyama wao wengine wote watakuwa wetu? Basi tukubali sharti lao, nao wataishi miongoni mwetu.” Neno: Maandiko Matakatifu Je, si mifugo yao, mali zao na wanyama wao wengine wote watakuwa wetu? Basi na tuwape kibali, nao wataishi miongoni mwetu.” BIBLIA KISWAHILI Je! Kondoo zao, na mali zao, na wanyama wao wote hawatakuwa mali zetu? Basi na tupatane nao tu, nao watakaa kwetu. |
Lakini kwa sharti hiyo moja tu watapatana nasi wakae wote kwetu, tuwe watu wamoja, kama tukitahiriwa kila mwanamume, kama wao walivyotahiriwa.
Wakawasikia Hamori na Shekemu mwanawe, wote watokeao katika lango la mji wake. Wakatahiriwa kila mwanamume, wote watokao katika lango la mji wake.
Mtu mwaminifu atakuwa na baraka tele; Lakini afanyaye haraka kuwa tajiri hakosi ataadhibiwa.
akawaambia wale waliokuwa wakiuza njiwa, Yaondoeni haya; msiifanye nyumba ya Baba yangu kuwa nyumba ya biashara.