Basi Abramu akahamisha hema yake, akaja na kukaa karibu na mialoni ya Mamre, nayo ni miti iliyoko Hebroni, akamjengea BWANA madhabahu huko.
Mwanzo 33:20 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Akajenga huko madhabahu, akaiita, El-elohe-Israeli. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Huko, akajenga madhabahu na kupaita Mungu ni Mungu wa Israeli. Biblia Habari Njema - BHND Huko, akajenga madhabahu na kupaita Mungu ni Mungu wa Israeli. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Huko, akajenga madhabahu na kupaita Mungu ni Mungu wa Israeli. Neno: Bibilia Takatifu Akajenga madhabahu pale na kupaita El-Elohe-Israeli. Neno: Maandiko Matakatifu Pale akajenga madhabahu na kupaita El-Elohe-Israeli. BIBLIA KISWAHILI Akajenga huko madhabahu, akaiita, El-elohe-Israeli. |
Basi Abramu akahamisha hema yake, akaja na kukaa karibu na mialoni ya Mamre, nayo ni miti iliyoko Hebroni, akamjengea BWANA madhabahu huko.
Akamwambia, Jina lako hutaitwa tena Yakobo, ila Israeli, maana umeshindana na Mungu, na watu, nawe umeshinda.
Akainunua sehemu ya nchi, alipopiga hema yake, kwa mkono wa wana wa Hamori, baba wa Shekemu, kwa vipande mia moja vya fedha.
Akajenga huko madhabahu, akapaita mahali pale, El-Betheli; kwa sababu huko Mungu alimtokea, hapo alipomkimbia ndugu yake.
Nuhu akamjengea BWANA madhabahu; akatwaa katika kila mnyama aliye safi, na katika kila ndege aliye safi, akavitoa sadaka za kuteketezwa juu ya madhabahu.
Kwa hiyo Daudi akamhimidi BWANA, mbele ya mkutano wote; naye Daudi akasema, Uhimidiwe, Ee BWANA, Mungu wa Israeli baba yetu, milele na milele.
Baba zetu waliabudu katika mlima huu, nanyi husema ya kwamba huko Yerusalemu ni mahali patupasapo kuabudia.