Yakobo akawaambia ndugu zake, Kusanyeni mawe. Wakatwaa mawe, wakafanya chungu, nao wakala huko karibu na ile chungu.
Mwanzo 31:45 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Yakobo akatwaa jiwe akalisimamisha kama nguzo. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Basi, Yakobo akachukua jiwe, akalisimika kama nguzo ya ukumbusho. Biblia Habari Njema - BHND Basi, Yakobo akachukua jiwe, akalisimika kama nguzo ya ukumbusho. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Basi, Yakobo akachukua jiwe, akalisimika kama nguzo ya ukumbusho. Neno: Bibilia Takatifu Hivyo Yakobo akachukua jiwe, akalisimamisha kama nguzo. Neno: Maandiko Matakatifu Hivyo Yakobo akachukua jiwe, akalisimamisha kama nguzo. BIBLIA KISWAHILI Yakobo akatwaa jiwe akalisimamisha kama nguzo. |
Yakobo akawaambia ndugu zake, Kusanyeni mawe. Wakatwaa mawe, wakafanya chungu, nao wakala huko karibu na ile chungu.
Yakobo akasimamisha nguzo mahali aliposema naye, nguzo ya mawe, akamimina juu yake sadaka ya kinywaji, akamimina mafuta juu yake.
Yoshua akayaandika maneno haya katika kitabu cha Torati ya Mungu; kisha akatwaa jiwe kubwa, akalisimamisha huko, chini ya ule mwaloni uliokuwa karibu na patakatifu pa BWANA.
Yoshua akawaambia watu wote, Tazama, jiwe hili litakuwa shahidi juu yetu; kwa maana limesikia maneno yote ya BWANA aliyotuambia, basi litakuwa shahidi juu yenu, msije mkamkana Mungu wenu.