Ikawa Raheli alipomzaa Yusufu, Yakobo akamwambia Labani, Nipe ruhusa niende kwetu, na kwenye nchi yangu.
Mwanzo 30:24 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Akamwita jina lake Yusufu, akisema, Bwana aniongeze mwana mwingine. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kwa hiyo akamwita mtoto huyo Yosefu akisema, “Mwenyezi-Mungu na aniongezee mtoto mwingine wa kiume.” Biblia Habari Njema - BHND Kwa hiyo akamwita mtoto huyo Yosefu akisema, “Mwenyezi-Mungu na aniongezee mtoto mwingine wa kiume.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kwa hiyo akamwita mtoto huyo Yosefu akisema, “Mwenyezi-Mungu na aniongezee mtoto mwingine wa kiume.” Neno: Bibilia Takatifu Akamwita jina Yusufu, akasema, “Mwenyezi Mungu na anipe mwana mwingine.” Neno: Maandiko Matakatifu Akamwita Yusufu na kusema, “bwana na anipe mwana mwingine.” BIBLIA KISWAHILI Akamwita jina lake Yusufu, akisema, Bwana aniongeze mwana mwingine. |
Ikawa Raheli alipomzaa Yusufu, Yakobo akamwambia Labani, Nipe ruhusa niende kwetu, na kwenye nchi yangu.
Hivi ndivyo vizazi vya Yakobo. Yusufu, aliyekuwa mwenye miaka kumi na saba, alikuwa akichunga kondoo pamoja na ndugu zake; naye alikuwa kijana pamoja na wana wa Bilha, na wana wa Zilpa, wake wa baba yake. Yusufu akamletea baba yao habari zao mbaya.
Ndugu zake wakaona ya kuwa baba yao anampenda kuliko ndugu zake wote, wakamchukia, wala hawakuweza kusema naye kwa amani.
Naye Yusufu alikuwa ni mkuu juu ya nchi, ndiye aliyewauzia watu wote wa nchi. Nao ndugu zake Yusufu wakaja, wakainama kifudifudi mbele yake.
Na wewe mwanadamu, twaa kijiti kimoja; ukaandike juu yake, Kwa Yuda, na kwa wana wa Israeli wenzake; kisha, twaa kijiti cha pili; ukaandike juu yake, Kwa Yusufu, kijiti cha Efraimu, na kwa nyumba yote ya Israeli wenzake;
Wa kabila la Zabuloni elfu kumi na mbili. Wa kabila la Yusufu elfu kumi na mbili. Wa kabila la Benyamini elfu kumi na mbili waliotiwa mhuri.