Isaka akamwomba BWANA kwa ajili ya mke wake, maana alikuwa tasa. Naye BWANA akamwitikia, na Rebeka mkewe akachukua mimba.
Mwanzo 30:22 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Mungu akamkumbuka Raheli; Mungu akamsikia, akamfungua tumbo. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kisha Mungu akamkumbuka Raheli, akalikubali ombi lake na kumjalia kupata watoto. Biblia Habari Njema - BHND Kisha Mungu akamkumbuka Raheli, akalikubali ombi lake na kumjalia kupata watoto. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kisha Mungu akamkumbuka Raheli, akalikubali ombi lake na kumjalia kupata watoto. Neno: Bibilia Takatifu Ndipo Mungu akamkumbuka Raheli, akasikia maombi yake na akafungua tumbo lake. Neno: Maandiko Matakatifu Ndipo Mungu akamkumbuka Raheli, akasikia maombi yake na akafungua tumbo lake. BIBLIA KISWAHILI Mungu akamkumbuka Raheli; Mungu akamsikia, akamfungua tumbo. |
Isaka akamwomba BWANA kwa ajili ya mke wake, maana alikuwa tasa. Naye BWANA akamwitikia, na Rebeka mkewe akachukua mimba.
BWANA akaona ya kwamba Lea hakupendwa, naye akafungua tumbo lake; bali Raheli alikuwa hazai.
Yakobo akamghadhibikia Raheli, akasema, Je! Mimi ni badala ya Mungu, aliyekuzuilia uzao wa mimba?
Na Mungu akamkumbuka Nuhu, na kila kilicho hai, na wanyama wote waliokuwamo pamoja naye katika safina; Mungu akavumisha upepo juu ya nchi, maji yakapungua;