Lea alipoona ya kuwa ameacha kuzaa, alimtwaa Zilpa, mjakazi wake, akampa Yakobo kuwa mkewe.
Mwanzo 29:35 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Akapata mimba tena, akazaa mwana. Akasema, Mara hii nitamsifu BWANA; kwa hiyo akamwita jina lake Yuda; akaacha kuzaa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Lea akapata mimba tena, akajifungua mtoto wa kiume, akamwita Yuda, akisema, “Safari hii nitamsifu Mwenyezi-Mungu.” Kisha Lea akaacha kuzaa. Biblia Habari Njema - BHND Lea akapata mimba tena, akajifungua mtoto wa kiume, akamwita Yuda, akisema, “Safari hii nitamsifu Mwenyezi-Mungu.” Kisha Lea akaacha kuzaa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Lea akapata mimba tena, akajifungua mtoto wa kiume, akamwita Yuda, akisema, “Safari hii nitamsifu Mwenyezi-Mungu.” Kisha Lea akaacha kuzaa. Neno: Bibilia Takatifu Akapata tena mimba, naye alipozaa mwana akasema, “Wakati huu nitamsifu Mwenyezi Mungu.” Kwa hiyo akamwita jina Yuda. Kisha akaacha kuzaa watoto. Neno: Maandiko Matakatifu Akapata tena mimba, naye alipozaa mwana, akasema, “Wakati huu nitamsifu bwana.” Kwa hiyo akamwita Yuda. Kisha akaacha kuzaa watoto. BIBLIA KISWAHILI Akapata mimba tena, akazaa mwana. Akasema, Mara hii nitamsifu BWANA; kwa hiyo akamwita jina lake Yuda; akaacha kuzaa. |
Lea alipoona ya kuwa ameacha kuzaa, alimtwaa Zilpa, mjakazi wake, akampa Yakobo kuwa mkewe.
Wana wa Zilpa, kijakazi wa Lea, ni Gadi na Asheri. Hawa ndio wana wa Yakobo aliozaliwa katika Padan-aramu.
Na wana wa Yuda; Eri, na Onani, na Shela, na Peresi, na Zera; lakini Eri na Onani walikufa katika nchi ya Kanaani. Na wana wa Peresi, ni Hesroni, na Hamuli.
Ingawa Yuda ndiye aliyekuzwa zaidi miongoni mwa nduguze, na kwake ndiko alikotoka mtawala; haki ile ya mzaliwa wa kwanza ilikuwa ya Yusufu);
Na mpakani mwa Reubeni, toka upande wa mashariki hadi upande wa magharibi; Yuda, fungu moja.
Katika wana wa Yuda, vizazi vyao, kwa kufuata jamaa zao, na nyumba za baba zao, kama hesabu ya majina, kuanzia umri wa miaka ishirini na zaidi, wote walioweza kwenda vitani;
Na baraka ya Yuda ni hii; akasema, Isikize, Ee BWANA, sauti ya Yuda, Umlete ndani kwa watu wake; Alijitetea kwa mikono yake; Nawe utakuwa msaada juu ya adui zake.