Kisha akaondoka huko akaenda mpaka mlima ulio upande wa mashariki wa Betheli, akaipiga hema yake; Betheli ilikuwa upande wa magharibi, na Ai upande wa mashariki, akamjengea BWANA madhabahu huko, akaliitia jina la BWANA.
Mwanzo 28:19 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Akaita jina la mahali pale Betheli; lakini jina la mji ule hapo kwanza uliitwa Luzu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Akapaita mahali hapo Betheli; lakini jina la awali la mji huo lilikuwa Luzu. Biblia Habari Njema - BHND Akapaita mahali hapo Betheli; lakini jina la awali la mji huo lilikuwa Luzu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Akapaita mahali hapo Betheli; lakini jina la awali la mji huo lilikuwa Luzu. Neno: Bibilia Takatifu Mahali pale akapaita Betheli, ingawa mji ule hapo awali uliitwa Luzu. Neno: Maandiko Matakatifu Mahali pale akapaita Betheli, ingawa mji ule hapo kwanza uliitwa Luzu. BIBLIA KISWAHILI Akaita jina la mahali pale Betheli; lakini jina la mji ule hapo kwanza uliitwa Luzu. |
Kisha akaondoka huko akaenda mpaka mlima ulio upande wa mashariki wa Betheli, akaipiga hema yake; Betheli ilikuwa upande wa magharibi, na Ai upande wa mashariki, akamjengea BWANA madhabahu huko, akaliitia jina la BWANA.
Akafika mahali fulani akakaa huko usiku kucha, maana jua lilikuwa limekuchwa; akatwaa jiwe moja la mahali pale akaliweka chini ya kichwa chake, akalala usingizi pale pale.
Mimi ni Mungu wa Betheli, huko ulikotia mafuta nguzo, na kuniwekea nadhiri. Sasa ondoka, toka katika nchi hii, urudi mpaka nchi ile uliyozaliwa.
Mungu akamwambia Yakobo, Ondoka, panda uende Betheli, ukakae huko; ukamfanyie Mungu madhabahu huko; yeye aliyekutokea ulipomkimbia Esau, ndugu yako.
Yakobo akasimamisha nguzo mahali aliposema naye, nguzo ya mawe, akamimina juu yake sadaka ya kinywaji, akamimina mafuta juu yake.
Basi Yakobo akafika Luzu, katika nchi ya Kanaani, ndio Betheli, yeye na watu wote waliokuwa pamoja naye.
Akajenga huko madhabahu, akapaita mahali pale, El-Betheli; kwa sababu huko Mungu alimtokea, hapo alipomkimbia ndugu yake.
Yakobo akamwambia Yusufu, Mungu Mwenyezi alinitokea huko Luzu, katika nchi ya Kanaani, akanibariki,
Eliya akamwambia Elisha, Tafadhali, kaa hapa; maana BWANA amenituma niende mpaka Betheli.
Abiya akamfuata Yeroboamu, akamnyang'anya miji, Betheli na vijiji vyake na Yeshana na vijiji vyake, na Efroni na vijiji vyake.
Ingawa wewe, Israeli, unafanya uzinzi, lakini asiasi Yuda; nanyi msiende Gilgali wala msipande mpaka Beth-aveni, wala msiape mkisema, Aishivyo BWANA.
kisha ikatoka huko Betheli kwendelea Luzu, kisha ikaendelea hata kuufikia mpaka wa Waarki mpaka Atarothi;
Kisha mpaka ukaendelea kutoka hapo na kufikia mji wa Luzu, ubavuni mwa Luzu (ndio Betheli), kwa upande wa kusini; kisha mpaka ukateremkia Ataroth-adari, karibu na mlima ulio upande wa kusini wa Beth-horoni wa chini.
Kisha akatwaa watu kama elfu tano, akawaweka kuotea kati ya Betheli na Ai, upande wa magharibi wa huo mji.
Ndipo wana wa Israeli wote, na hao watu wote, wakakwea, wakaenda Betheli, na kulia, wakaketi hapo mbele za BWANA, wakafunga siku hiyo hadi jioni; nao wakasongeza sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani mbele za BWANA.
Kisha utakwenda mbele kutoka hapo, na kufika kwenye mwaloni wa Tabori, na hapo watu watatu watakutana nawe, wanaokwea kumwendea Mungu huko Betheli, mmoja anachukua wana-mbuzi watatu, na mwingine anachukua mikate mitatu, na mwingine anachukua kiriba cha divai;
Naye huenda mwaka kwa mwaka kuzunguka mpaka Betheli, na Gilgali, na Mispa; akawaamua katika miji yote ya Israeli.