Naye akasema, Ee BWANA, Mungu wa bwana wangu Abrahamu, nakuomba mambo yangu uyajalie yawe heri leo, ukamfadhili bwana wangu Abrahamu.
Mwanzo 27:20 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Isaka akamwuliza mwanawe, Imekuwaje umepata upesi namna hii, mwanangu? Akasema, Kwa sababu BWANA, Mungu wako, amenifanikisha. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Lakini Isaka akamwuliza, “Imekuwaje umepata mawindo upesi hivyo, mwanangu?” Yakobo akamjibu, “Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, amenifanikisha.” Biblia Habari Njema - BHND Lakini Isaka akamwuliza, “Imekuwaje umepata mawindo upesi hivyo, mwanangu?” Yakobo akamjibu, “Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, amenifanikisha.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Lakini Isaka akamwuliza, “Imekuwaje umepata mawindo upesi hivyo, mwanangu?” Yakobo akamjibu, “Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, amenifanikisha.” Neno: Bibilia Takatifu Isaka akamuuliza mwanawe, “Umepataje mawindo haraka hivi, mwanangu?” Akajibu, “Mwenyezi Mungu, Mungu wako, amenifanikisha.” Neno: Maandiko Matakatifu Isaka akamuuliza mwanawe. “Umepataje haraka namna hii, mwanangu?” Akajibu, “bwana Mwenyezi Mungu wako amenifanikisha.” BIBLIA KISWAHILI Isaka akamwuliza mwanawe, Imekuwaje umepata upesi namna hii, mwanangu? Akasema, Kwa sababu BWANA, Mungu wako, amenifanikisha. |
Naye akasema, Ee BWANA, Mungu wa bwana wangu Abrahamu, nakuomba mambo yangu uyajalie yawe heri leo, ukamfadhili bwana wangu Abrahamu.
Isaka akamwambia Yakobo, Karibu, tafadhali, ili nikupapase, mwanangu, nione kwamba wewe ndiwe mwanangu Esau, ama siyo.
Je! Mtanena yasiyo ya haki kwa ajili ya Mungu, Na kusema kwa udanganyifu kwa ajili yake?
Usilitaje bure jina la BWANA, Mungu wako, maana BWANA hatamhesabia kuwa hana hatia mtu alitajaye jina lake bure.