Kisha Abrahamu akamlaumu Abimeleki kwa sababu ya kisima cha maji ambacho watumishi wa Abimeleki wamemnyang'anya.
Mwanzo 26:15 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Na vile visima vyote walivyochimba watumwa wa baba yake, siku za Abrahamu babaye, Wafilisti walikuwa wamevifukia, wakavijaza udongo. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wafilisti walikuwa wamevifukia visima vyote vya maji ambavyo watumishi wa Abrahamu, baba yake, walikuwa wamechimba wakati alipokuwa bado hai. Biblia Habari Njema - BHND Wafilisti walikuwa wamevifukia visima vyote vya maji ambavyo watumishi wa Abrahamu, baba yake, walikuwa wamechimba wakati alipokuwa bado hai. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wafilisti walikuwa wamevifukia visima vyote vya maji ambavyo watumishi wa Abrahamu, baba yake, walikuwa wamechimba wakati alipokuwa bado hai. Neno: Bibilia Takatifu Kwa hiyo visima vyote vilivyochimbwa na watumishi wakati wa Ibrahimu baba yake, Wafilisti wakavifukia, wakavijaza udongo. Neno: Maandiko Matakatifu Kwa hiyo visima vyote vilivyochimbwa na watumishi wakati wa Ibrahimu baba yake, Wafilisti wakavifukia, wakavijaza udongo. BIBLIA KISWAHILI Na vile visima vyote walivyochimba watumwa wa baba yake, siku za Abrahamu babaye, Wafilisti walikuwa wamevifukia, wakavijaza udongo. |
Kisha Abrahamu akamlaumu Abimeleki kwa sababu ya kisima cha maji ambacho watumishi wa Abimeleki wamemnyang'anya.
Akasema, Hawa wana-kondoo saba majike utawapokea mkononi mwangu, wawe ushuhuda ya kuwa ni mimi niliyekichimba kisima hiki.