Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Mwanzo 25:8 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

Abrahamu akafariki, naye akafa katika uzee mwema, mzee sana, ameshiba siku, akakusanyika kwa watu wake.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Alifariki baada ya kuishi maisha marefu na ya fanaka, akajiunga na wazee wake waliomtangulia.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Alifariki baada ya kuishi maisha marefu na ya fanaka, akajiunga na wazee wake waliomtangulia.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Alifariki baada ya kuishi maisha marefu na ya fanaka, akajiunga na wazee wake waliomtangulia.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Ndipo Ibrahimu akapumua pumzi ya mwisho na akafa akiwa mwenye umri mzuri, mzee aliyeshiba siku; naye akakusanywa pamoja na watu wake.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Ndipo Ibrahimu akapumua pumzi ya mwisho na akafa akiwa mwenye umri mzuri, mzee aliyeshiba siku, naye akakusanywa pamoja na watu wake.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Abrahamu akafariki, naye akafa katika uzee mwema, mzee sana, ameshiba siku, akakusanyika kwa watu wake.

Tazama sura
Tafsiri zingine



Mwanzo 25:8
27 Marejeleo ya Msalaba  

Lakini wewe utakwenda kwa baba zako kwa amani, utazikwa katika uzee mwema.


Ishmaeli aliishi miaka mia moja na thelathini na saba. Akakata roho, akafa, akakusanyika kwa watu wake.


Abrahamu aliishi miaka mia moja na sabini na mitano.


Ikawa hapo katika kutoa roho yake, maana alikufa, akamwita jina lake Benoni, lakini babaye alimwita Benyamini.


Wanawe wote, na binti zake wote, wakaondoka wamtulize, lakini akakataa kutulizwa, akasema, La! Nitashuka kaburini kwa mwanangu, nikiomboleza. Basi baba yake akamlilia.


Akawaamuru, akasema, Mimi ninakwenda kukusanywa pamoja na watu wangu; mnizike pamoja na baba zangu, katika pango iliyomo shambani mwa Efroni, Mhiti;


Basi Yakobo alipokwisha kuwaagiza wanawe, akakunja miguu yake kitandani, akafa, akakusanywa pamoja na watu wake.


kwa kuwa wanawe wakamchukua mpaka nchi ya Kanaani, na wakamzika katika pango ya shamba la Makpela, iliyo mbele ya Mamre, aliyoinunua Abrahamu pamoja na shamba kwa Efroni Mhiti, pawe milki yake ya kuzikia.


Basi Daudi alipokuwa mzee kwa kuishi siku nyingi; alimtawaza mwanawe Sulemani awe mfalme wa Waisraeli.


Akafa akiwa mzee sana, mwenye maisha marefu, mali na heshima; naye Sulemani mwanawe akatawala badala yake.


Lakini Yehoyada akawa mzee, mwenye siku nyingi, akafa; alipokufa alikuwa na umri wa miaka mia moja na thelathini.


Hufanya mapito yake kung'aa nyuma yake Hata mtu angedhani kilindi kina mvi.


Basi Ayubu akafa, akiwa mzee sana mwenye kujawa na siku.


Utafika kaburini mwenye umri mtimilifu, Kama mganda wa ngano ulivyo wakati wake.


Fahari ya vijana ni nguvu zao, Na uzuri wa wazee ni kichwa chenye mvi.


Lakini nimejaa ghadhabu ya BWANA; nimechoka kwa kujizuia; imwageni juu ya watoto walio njiani, na juu ya kusanyiko la vijana pia; maana hata mume atatwaliwa pamoja na mkewe, mzee pamoja na yeye aliyetimiza siku zake.


Haruni atakusanywa awe pamoja na watu wake; kwa kuwa hataingia katika nchi niliyowapa wana wa Israeli, kwa sababu mliasi kinyume cha neno langu hapo penye maji ya Meriba.


Na ukiisha kuiona, wewe nawe utakusanyika pamoja na baba zako, kama Haruni ndugu yako alivyokusanyika;


Mara malaika wa Bwana akampiga, kwa sababu hakumpa Mungu utukufu; akaliwa na wadudu, akatokwa na roho.


Kwa maana Daudi, akiisha kulitumikia shauri la Mungu katika kizazi chake, alilala, akawekwa pamoja na baba zake, akaona uharibifu.


Mara akaanguka miguuni pake akafa; wale vijana wakaingia wakamkuta amekufa, wakamchukua nje, wakamzika pamoja na mumewe.


Anania aliposikia maneno haya akaanguka, akafa. Hofu nyingi ikawapata watu wote walioyasikia haya.


ukafe katika kilima, huko ukweako, ukusanywe uwe pamoja na jamaa zako; kama alivyokufa nduguyo Haruni katika mlima wa Hori, akakusanywa awe pamoja na watu wake;


Tena watu wote wa kizazi hicho nao walikusanywa waende kwa baba zao; kikainuka kizazi kingine nyuma yao, ambacho hakikumjua BWANA, wala hawakuijua hiyo kazi ambayo alikuwa ameitenda kwa ajili ya Israeli.


Basi Gideoni mwana wa Yoashi akafa mwenye umri wa uzee mwema, akazikwa katika kaburi la Yoashi baba yake, katika Ofra ya Waabiezeri.