Isaka akatoka ili kutafakari shambani wakati wa jioni; akainua macho yake, akaona, kuna ngamia wanakuja.
Mwanzo 24:64 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Rebeka akainua macho, naye alipomwona Isaka, alishuka juu ya ngamia. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Naye Rebeka alipotazama na kumwona Isaka, alishuka chini Biblia Habari Njema - BHND Naye Rebeka alipotazama na kumwona Isaka, alishuka chini Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Naye Rebeka alipotazama na kumwona Isaka, alishuka chini Neno: Bibilia Takatifu Rebeka pia akainua macho, akamwona Isaka. Akashuka kutoka ngamia wake, Neno: Maandiko Matakatifu Rebeka pia akainua macho akamwona Isaka. Akashuka kutoka kwenye ngamia wake BIBLIA KISWAHILI Rebeka akainua macho, naye alipomwona Isaka, alishuka juu ya ngamia. |
Isaka akatoka ili kutafakari shambani wakati wa jioni; akainua macho yake, akaona, kuna ngamia wanakuja.
Akamwambia mtumishi, Ni nani mtu huyu ajaye shambani kutulaki? Mtumishi akasema, Huyu ndiye bwana wangu. Basi akatwaa shela yake akajifunika.
Kisha ikawa, hapo huyo mwanamke alipokwenda kwa mumewe, akamtaka aombe shamba kwa baba yake; akashuka katika punda wake; Kalebu akamwuliza, Unataka nikupe nini?
Ikawa hapo alipokwenda kukaa naye, huyo mwanamke akamtaka ili aombe shamba kwa baba yake; na huyo mwanamke akashuka katika punda wake; Kalebu akamwuliza, Una haja gani utakayo?