Naye akamtendea Abramu mema kwa ajili yake; naye alikuwa na kondoo na ng'ombe, na punda dume, na watumwa, na wajakazi, na punda majike, na ngamia.
Mwanzo 24:35 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC na BWANA amembarikia sana bwana wangu, amekuwa mtu mkuu; amempa kondoo, na ng'ombe, na fedha, na dhahabu, na watumishi, na wajakazi, na ngamia, na punda. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mwenyezi-Mungu amembariki sana bwana wangu, naye amekuwa mtu maarufu. Amempa makundi ya kondoo na mifugo mingi, fedha na dhahabu, watumishi wa kiume na wa kike, ngamia na punda! Biblia Habari Njema - BHND Mwenyezi-Mungu amembariki sana bwana wangu, naye amekuwa mtu maarufu. Amempa makundi ya kondoo na mifugo mingi, fedha na dhahabu, watumishi wa kiume na wa kike, ngamia na punda! Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mwenyezi-Mungu amembariki sana bwana wangu, naye amekuwa mtu maarufu. Amempa makundi ya kondoo na mifugo mingi, fedha na dhahabu, watumishi wa kiume na wa kike, ngamia na punda! Neno: Bibilia Takatifu Mwenyezi Mungu amembariki sana bwana wangu, amekuwa tajiri. Amempa kondoo na ng’ombe, fedha na dhahabu, watumishi wa kiume na wa kike, ngamia na punda. Neno: Maandiko Matakatifu bwana amembariki sana bwana wangu, amekuwa tajiri. Amempa kondoo na ng’ombe, fedha na dhahabu, watumishi wa kiume na wa kike, ngamia na punda. BIBLIA KISWAHILI na BWANA amembarikia sana bwana wangu, amekuwa mtu mkuu; amempa kondoo, na ng'ombe, na fedha, na dhahabu, na watumishi, na wajakazi, na ngamia, na punda. |
Naye akamtendea Abramu mema kwa ajili yake; naye alikuwa na kondoo na ng'ombe, na punda dume, na watumwa, na wajakazi, na punda majike, na ngamia.
nami nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, na kukubariki, na kulikuza jina lako; nawe uwe baraka;
nami nitawabariki wakubarikio, naye akulaaniye nitamlaani; na katika wewe jamaa zote za dunia watabarikiwa.
Basi Abrahamu alikuwa mzee mwenye miaka mingi, na BWANA alikuwa amembariki Abrahamu katika vitu vyote.
Ikawa, baada ya kufa kwake Abrahamu, Mungu akambariki Isaka mwanawe. Naye Isaka akakaa karibu ya Beer-lahai-roi.
Kwa hiyo mtu huyo akazidi mno, akawa na wanyama wengi, na vijakazi, na watumwa, na ngamia, na punda.
Naam, kwa Mungu wa baba yako atakayekusaidia; Kwa baraka za juu mbinguni. Baraka za vilindi vilivyo chini, Baraka za maziwa, na za mimba.
Mali yake nayo ilikuwa ni kondoo elfu saba, na ngamia elfu tatu, na jozi za ng'ombe mia tano, na punda wake mia tano, na watumishi wengi sana; basi hivi mtu huyo alikuwa ni mkuu sana kuliko watu wote wa upande wa mashariki.
Nawe umenipa ngao ya wokovu wako, Mkono wako wa kulia umenitegemeza, Na unyenyekevu wako umenikuza.
Lakini, mtumwa yule akisema moyoni mwake, Bwana wangu anakawia kuja, akaanza kuwapiga watumwa wenzake, wanaume kwa wanawake, akila na kunywa na kulewa;
Maana, mazoezi ya viungo vya mwili yana manufaa kidogo, lakini utauwa una manufaa ya kila aina; yaani, unayo ahadi ya uzima wa sasa, na ya ule utakaokuwapo baadaye.