Mwanzo 23:18 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC kuwa mali yake Abrahamu, mbele ya wazawa wa Hethi, mbele ya watu wote waingiao katika mlango wa mji wake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Abrahamu mbele ya Wahiti wote waliokutanika penye lango la mji. Biblia Habari Njema - BHND Abrahamu mbele ya Wahiti wote waliokutanika penye lango la mji. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Abrahamu mbele ya Wahiti wote waliokutanika penye lango la mji. Neno: Bibilia Takatifu kwa Ibrahimu kuwa mali yake mbele ya Wahiti wote waliokuwa wamekuja kwenye lango la mji. Neno: Maandiko Matakatifu kwa Ibrahimu kuwa mali yake mbele ya Wahiti wote waliokuwa wamekuja kwenye lango la mji. BIBLIA KISWAHILI kuwa mali yake Abrahamu, mbele ya wazawa wa Hethi, mbele ya watu wote waingiao katika mlango wa mji wake. |
Basi Efroni alikuwa akiketi kati ya wazawa wa Hethi. Efroni Mhiti akamjibu Abrahamu, na wazawa wa Hethi wanasikiliza, hata watu wote waingiao mlango wa mji wake, akisema,
Basi baada ya hayo Abrahamu akamzika Sara mkewe katika pango la shamba la Makpela kuelekea Mamre, ndiyo Hebroni, katika nchi ya Kanaani.
Isaka na Ishmaeli wanawe wakamzika katika pango ya Makpela, katika shamba la Efroni mwana wa Sohari Mhiti, lielekealo Mamre.
Hamori, na Shekemu mwanawe, wakaja langoni pa mji wao, wakasema na watu wa mji wao, wakinena,
Wakawasikia Hamori na Shekemu mwanawe, wote watokeao katika lango la mji wake. Wakatahiriwa kila mwanamume, wote watokao katika lango la mji wake.
na ile hati ya kununua nikampa Baruku, mwana wa Neria, mwana wa Maaseya, mbele ya uso wa Hanameli, mwana wa mjomba wangu, na mbele ya mashahidi wale walioitia sahihi hati ya kununua, mbele ya Wayahudi wote walioketi katika ukumbi wa walinzi.
Basi Boazi akakwea kwenda mpaka langoni, akaketi pale; na tazama, yule mtu wa jamaa aliyekuwa karibu, ambaye Boazi amemnena, akapita. Naye akamwita, Haya! Wewe, karibu, uketi hapa. Naye akaja akaketi.